Salaam wanajamii,
Ninaomba kuuliza maswali yafuatayo:
1:Hivi naweza kuchimba madini nikiwa na primary mining licence bila kuwa na mining licence?
2:Kama nina primary mining licence ni hatua zipi ninapaswa kuzichukua mpaka niweze kuchimba?
3:Je kwa mtu mwenye primary mining licence ni muda gani anaweza kukaa bila kulitumia eneo na ikapelekea yeye kunyang'anywa leseni au ni mambo gani asipoyafanya itapelekea yeye kufutiwa leseni?
4:Ni hatua zipi kisheria natakiwa kuzifuata kufungua ofisi ya kushughulikia maeneo ya madini yaliyokatiwa primary mining licence.
Wataalamu tafadhali naomba mnijuze.Samahani kama nitakuwa nimejichanganya kidogo kwenye kuuliza aya maswali.
Natumai nimeeleweka.Karibuni..!