Msaada wa kisheria kuhusu mali za baba yangu

The oris

Member
Jan 4, 2017
91
167
Habari za jioni ? Nilikuwa naomba msaada wa mali za baba yangu kwa sababu ndugu zangu naona hawana mpango wa kufatilia.
Nifupishe kidogo hii habari yangu, mwaka 2006 baada ya baba kuachana na mama 'baba aliamua kuoa mke mwingine wakati huo nilikuwa na miaka 12 nilikuwa naishi kijijini kwa babu.
Kipindi baba wakati anaoa alikuwa hana uwezo wowote lakini alipokuja kuokoka/mlokole mambo yake yakaanza kunyooka alijenga nyumba ya kawaida na alinunua gari na vilevile alikuwa na shamba ekari 100. Shamba pamoja nyumba vyote navijua vilipo , tuseme kipindi iko nilikuwa na akili za utoto sikuweza kujua mambo ya hati za nyumba wala shamba na gari nilikuwa na chukulia kawaida tu .nakingine mzee alikuwa msiri kwa ndugu zake ili nalo lilikuwa tatizo pia .

Mwaka 2009 kipindi nipo kidato cha kwanza mwezi wa pili baba alifariki dunia, lakini siku mbili nyuma kabla hajafariki alikuwa akinisihi sana nikaonane nae ili aweze kuniandikisha mali zake.wakati naenda kumuona kesho nikaambiwa mzee amefariki.
Tukafanya taratibu zote za mazishi tukazika , arobaini ilivyo malizika nikarudi kijijini kuendelea na masomo.
Ndugu zangu kwa upande wa baba walianza kufatilia mali lakini wakaambiwa kuwa baba alikuwa hana mali yoyote coz nyumba zote mbili , gari na shamba ni mali ya kanisa kwahiyo mzee hana mali yoyote ile.
Ndugu wakaamua kuacha kufatilia na kipindi iko nilikuwa sijali kuhusu mali za mzee nilikuwa nipo nipo tu nahisi sababu nilikuwa bado mdogo sijui lolote.
Hivi sasa nina miaka 22 ni mtu mzima najitambua kabisa nataka nianze kufatilia mali za baba yangu.
Wataalamu wa sheria naombeni msaada wenu kwa sababu sijui pakuanzia na kipindi kirefu kidogo kimepita tangu mzee afariki.
NB:nimefupisha hii habari kama kuna mwanasheria ameamua kunisaidia naomba aje PM kwa maswali zaidi, sitaki kuweka data zote coz ndugu zangu wengi wapo humu jamii forum.
Kwa vile wameshindwa kufuatilia nataka nifatilie mwenyewe
 
ndugu nakushauri uongeze juhudi kwenye masomo Mungu atakubariki utabata vyako achana na mambo ya urithi, baba yangu alifariki 1994 katika uhai wake alimiliki nyumba na viwanja vingi hapa dar ila alipofariki wadogo zake waliuza nyumba na mali zote hawakuwahi kutununulia hata soksi za shule, nakumbuka mama alikua akituambia Mungu atawapa zenu na leo hii wale ndugu zetu wanatutafuta!
 
Hapo mliuzwa tu , ndugu zako waligawana mali ukaambiwa za kanisa. Piga kitabu bado umri ni mdogo achana na hizo mambo maisha na mitihani changamoto lazima pambana dogo.
 
dogo komaa upate haki yako usitishwe kwa kupewa vitisho vya kumwaga damu...kila mtu atakufa tu na Mungu ndiye mpangaji wa yote...subiri wataalamu waje wakusaidie
sagaci Francis12
 
Back
Top Bottom