Msaada wa kisheria: Hivi ni lazima kila anayekamatwa na polisi aswekwe rumande?

oyaoya

JF-Expert Member
Mar 4, 2012
277
39
Wakuu,
Nimeshuhudia jamaa kadhaa wakikamatwa hata na makosa madogo madogo (mengine ya kusingiziwa) wanapopelekwa polisi huswekwa rumande (lockup) kabla hata ya kuandikishwa maelezo wala kujitetea... mmoja aliwahi kuzuiliwa kwenda kazini bila ya sababu zozote kwa kosa ambalo baadae ilikuja kugundulika kuwa yeye si muhusika.
  1. Sheria inasemaje kuhusu sababu za mtu kuswekwa rumande wakuu?
  2. Mtuhumiwa anawezaje kujiwekea dhamana ama kuomba arudi baadae kituoni kwa ajili ya kukamilisha baadhi ya mambo muhimu yanayomhusu hasa ya kikazi kabla ya kuja kuwekewa dhamana na mtu yeyote kama hajatoa taarifa kwa yeyote?
 
Back
Top Bottom