Msaada wa kisaikolojia

Oya wazee mnanipasua kichwa bhana.

Mtoa maada kaanza na VVU huku mbele siasa
Mara midege ya super 61 ya Hollywood huko.
Mara barakoa nini? Hii maana yake nini?
 
Habari za siku mbili tatu na poleni kwa msiba wa Bw. Mbele na wapendwa wetu wengine, ni jambo la kuhuzunisha sana.

Nimesoma ujumbe wa Bush na kuona kwamba anahitaji faraja na msaada wa KISAIKOLOJIA, tukimwacha hivyo haitakuwa sawa.

Mtu anapopatwa na msiba au jambo kubwa la kushtua anapitia hatua kadhaa ikiwemo:
1. Mshtuko (shock) wengine wanaweza kuzirai hata kupoteza maisha;
2. Kukataa (denial), "Sio kweli, wamekosea, sio yeye, amelala tu ataamka)
3. Hasira (anga), why me? Km ni VVU hapa mtu huambukiza wengine kwa makusudi (tufe wengi)
4. Woga (nina VVU nitakufa, fulani nitaishije bila yy)
5. Kujitenga (kujinyanyapaa) (hataki kuchangamana akidhaini wanamesema au wanamcheka)
6. Kubembeleza (bargaining) (Mungu ukimrudisha au ukiniepusha na hilo nita...) Hapa wengi hukimbilia kwa watoa faraja kama za kiroho
7. Kukubali hali au kuishi kwa matumani. Hapa mhusika anakubali kwamba yamekuwa na hakuna jinsi zaidi ya kukubali na kuendelea na maisha.

Kauli za mdogo na rafiki yangu Bush, "Bora niache kazi" na nyinginezo zinaaahiria kwamba yupo kwenye hatua mojawapo kati ya hizo.

Kuwa kwenye hatua ya kwanza hadi ya tano kimaweza kuleta madhara kwa mfusika au mtu/watu wengine.

Jukumu la mtaalamu ni kumsaidia mhusika kuvuka kutoka hatua moja hadi nyingine mpaka kuishi kwa matumaini.

Japo nitaongea na Bush, nashauri nyie MAAFISA UTAWALA, wenye dhamana ya ustawi wa wale mnaotuongoza mwendelee na juhudi za kumsaidia mwenzetu na sote tunaohitaji msaada wa kitaalamu wa kuvuka katika vipindi vya "GREEFING" au majonzi.

Kwa yeyote atakayehitaji msaada tuwasiliane nomwongoze kuhusu upatikaji wa huduma hiyo.

Nipo mtaani nashangashangaa maisha.
Mku hbr.
Mimi nimeangaikia hii huduma nimekosa kwani mara ya mwisho nilienda Osha kuulizia kama wanatoa hii huduma nikaambiwa hawatoi.
 
Anafanya tuamini kwamba Mungu wa kanisani na msikitini ni chaguo la mwisho baada ya kuhangaika hapa na pale.

Kwa kweli, viongozi wa dini wanajukumu kubwa la kutenganisha kati ya majukum ya Mungu kiroho na kimwili.

Wachore mstari kati ya masuala ya kiroho na kimwili.

Uongo wa kusema kwamba Mungu anaponya kila aina ya maradhi huku wao wamevaa barakoa kujikinga na Korona.

Hii ina ashiria kwamba hawana imana kuwa Mungu hawezi kuwakinga kwa maombi.

Kwa ufupi Bush wako anawatupia lawama viongozi wa dini kwanini wahubiri vitu wasivyoviishi.


Yule kikongwe katika taifa lile, aliweka wazi tu... Kwamba Mungu ana mambo mengi ya kufanya. Hawezi kudeal na uzembe wako wa kutofuata maelekezo.
 
Back
Top Bottom