Msaada wa kimawazo

lonely girl

Member
Joined
Sep 21, 2017
Posts
12
Reaction score
5
Habari za usiku!

Nimekuja mbele zenu ndugu zangu nikiomba mawazo yenu na ushauri wenu kwenye hili tatizo linalotesa nitesa sana.

Mimi ni mwanamke nilie kwenye late 20's na kwasasa nipo kwenye mahusiano na mwanaume ambae yupo kwenye 30+ na to be honest nampenda kweli huyu mwanaume na nilikua tayari kuishi nae kwenye hali yoyote Ile ila kwa sasa imefikia point najiona kwenda kufail na uvumilivu kufika mwisho ingawa bado sijakata tamaa.

Na mwanzoni alinijengea mazingira ya kumtrust na kweli within a short time nilimuamini sana na kujiona now nipo kwenye safe side.

Tulipanga mipango mingi ya kimaisha ingawa hadi sasa hakuna hata moja lililotekeleza na zaidi zaidi mimi ndio nimekua muhanga na hadi kunifanya niombe ushauri wenu.

Tangu nimeanza relation na huyu mwenzangu mimi ndio nimekua provider, akiwa kaishiwa akiniomba pesa huwa sina tatizo akiomba nampa, mda mwingine ataniambia nikopeshe nampa lkn sikua naona ni vibaya sababu najua kwenye relation kusaidiana kupo na kuna mda mambo huwa hayawi mazuri

But kitu nilichokua kugundua baadae huyu mwenzangu ni selfish sana yeye akiwa na tatizo anataka soon umsaidie ila mimi hata siku moja hajawahi nisaidia chochote hata uwe na tatizo vipi ukimwambia anaweza asijibu yani in short hajawahi nisaidia kwa lolote lile.

Kinachoniuma zaidi na kunitesa alinifanya niingie kwenye deni ili kufanikisha issue fulani aliyoiplan yeye na mimi niliona ni ya msingi na profitable kumbe ni hewa haipo baada tu ya kumkabidhi pesa sijaona chochote na sijui pesa alipeleka wapi.

Nimejaribu kwa mda mrefu kuongea nae hata kama alikua na tatizo basi pesa ya watu niliyochukua tuirudishe but amekua akikwepa na kunipa ahadi hewa kila siku na huku mimi nasumbuliwa sana nirudishe pesa za watu.

Nnachoumia zaidi mwenzangu kipato chake ni kikubwa, kimaisha yupo mbele sana zaidi yangu lkn amekua ananinyonya mimi bila huruma na kunisababishia madeni ambayo hata pesa sijui ilienda wapi na ilifanya nini.

Kitu kingine kinachoniumiza huyu mwenzangu ni mtu ambae hajali kabisa uwepo wangu, hana mda wa kukaa na mimi, hata nimuombe tukae kwa mda mfupi ataishia kuniambia niko busy na kazi, yani hata awe free vipi nikiingizia tu swala la kukaa na tuzungumze lazima alete sababu inabidi tu niwe mpole na kumsikiliza yeye.

Ila kinachonishangaza yeye huishia kaniambia siwezi kuachana na wewe na wewe ndio mke wangu na hata hata itokee nimpe maneno makali vipi hajawahi kureact negatively na suala la mawasiliano kwenye simu yupo so active na huwa ananiambia tu ipo siku yote yataisha.

Kiukweli nimejikuta nipo njia panda maumivu nayapata sana na nnateseka sana lkn kwa upande mwingine nikiangalia huyu mwenzangu hajawahi kuonyesha kama hanitaki na kila siku haachi kuniambia ananipenda.

Naombeni ushauri wenu wa kimawazo may be kuna watu waliwahi kutana na situation kama yangu, nipo kwenye kipindi kigumu sana, msongo wa mawazo umekua ni mkubwa sana hadi najikuta hata mambo mengine nashindwa kabisa kuyafanya.
 
Wajinga ndio waliwao yani mtu kakuzidi kipato lkn bado ww unakopa halaf unampa yeye?!


Ukweli ni kuwa siku ya mwisho utakuja kulia machozi ya damu maana utaachwa vibaya sana


Sisi wanaume tunapenda mteremko sana be very careful from now on usijipe asilimia zote kuwa utaolewa hapo au hiyo tabia itaisha
 
Mmmmm, kwamjibu wa maelezo yako Jamaa ni mnyonyaji, hakuna issue ya kukupima hapo!!
 
Pole dada. Watu selfish ni ngumu kuwaelewa.But be careful jamaa anaonekana yuko kimaslahi no matter kwamba anapretend to (care?)
 
shogangu niskilize mimi utalia zaid ya hapo ukiolewa !najua kwassa huwez nielewa kbs ! huyo hakawii kununua kiatu cha laki 2 wewe asikununulie ht yeboyebo za 3000! niamini haya ! wepesi kweli kuomba pesa kwa wake zao wakiwa nazp hawakukumbuki !

ni hayo tu! utanikumbuka
 
Shukrani
 
Huyo jamaa sawa na upele kwa asiye na kucha.

Kumbe wife material wapo ila tunapishana nao.
 
Kama mwanamke anampeda mwanaume j
kweli hangempina vile. S
Angeanza kuonyesha upendo kwa kuzingatia kipato cha mama kipo juu. Naona kama kuna dharau ya kimyakimya. Kama hatabadilika mapema mwanaume achia ngazi kwani wapo wenye upendo. Au umesita kwa kua kipato chake ni juu??
 
Hapana ingekua naangalia kipato chake mda mrefu ningeachana nae coz sijawahi faidika na chochote ila nilimuingiza sana moyoni
 
Sawa lakini hata Biblia imeandikwa kua wanawake tuishi nao kwa kutumia akili ya hali ya juu. Muombe Mola akupe hiyo akili
 
DADA YANGU POLE.

MIMI NI MWANAUME, NIKUELEZE TU UKWELI, HUYO HANA MPANGO WA KUWA NA WEWE. ANAKUTUMIA KUKAMILISHA YAKE. AKMALIZA ANAKUTUA.

UMRI WAKO NI MDOGO LAKN NI MKUBWA VILEVILE. FANYA MAAMUZ, TAFUTA MTU MWINGNE.
 
Aisee we dada kuwa makini sana,huyo jamaa anakuchuna. Na atakuchuna kweli kweli,hana huruma na wewe,hana muda na wewe,hayo mapenzi yanatoka wapi sasa? Stuka unapenda usipopendwa, na jamaa anakutumia kutimiza matakwa yake binafsi,yawezekana unachotoa wanaenda kuhongwa wenzako lonely girl
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…