Msaada wa kimawazo ndugu zangu kuhusu maisha

Msaada wa kimawazo ndugu zangu kuhusu maisha

eskobas2016

Member
Joined
Jul 14, 2016
Posts
71
Reaction score
31
Habari za majukumu ndugu zangu,

Natumai wazima wote,

Sina ndugu wa kuomba ushauri zaidi ya rafiki zangu wa JF kwani kwangu JF ni zaidi ya ndugu, rafiki, na jirani zangu.

Naombeni ushauri wenu,

Ni kwamba nimekuwa naishi home kwa takribani miaka mitano sasa huku nikiwa ndiye kila kitu hapa kwetu, yaani ninatoa mahitaji yote muhimu, huku nikiwa na wadogo zangu sita na wazazi pia, nima umri wa miaka kama 34 hivi, ila kwa sasa nilikuwa nahitaji kutoka na kuanza maisha yangu.

Nimezunguuka kwenye nyumba kadhaa za kupanga na kukuta nyumba ya kiwango nitachohitaji si chini ya laki mbili hadi tatu kwa mwezi, ambayo kwa mwaka kwa rent ya 250 ni sawa na 3,000,000, na hapo hapo itabidi niwe na saidia home kila siku kuacha kama elfu sita ivi, mshahara wangu ni laki sita kwa mwezi huku nikiwa na vijibiashara ninavyoingiza kama laki kwa mwezi, ila nikachekecha wazo hilo nikaona kama maisha yatakuwa magumu sana kwangu.

Ila hapa kwetu ninapoishi Tabata Segerea mbele ya nyumba yetu kuna kiwanja ambacho naweza jenga chumba kimoja cha kuishi na nikaungana na mke wangu huku tukijipanga kujenga nyumba yetu huko Gongo la mboto ambako nina kiwanja changu.

Ushauri ninaoomba kwenu ndugu zangu ni kuwa je;

1. Nihame na kutafuta sehemu nipange na kuishi na mke wangu.
2. Nijenge hata chumba kimoja niishi hapa hapa home Tabata huku. nikiwa najipanga kujenga kwangu.
3. Niishi tu nyumba moja na wazazi huku nikiwa najenga kwangu yaani. pesa yote niitumie kwenye kujenga kwangu.

PLEASE NAOMBA USHAURI WENU rafiki zangu.
 
Kaka ni vema ukaanza kujenga huko gombz, halafu uhamie mapema, sio lazima nyumba iishe yote, unaweza ukamaliza upande mmoja(hata kama ni chumba kimoja), then vingine ukamalizia baadaye ukiwa vizuri....hiyo ndiyoo shortcut muhimu......
 
Siku zote maamuzi sahihi huletwa na mipango sahihi! Angali gharama za maisha, kipato na matumizi yako kwa ujumla.

Cha muhimu ni bora hiyo Pesa ya kupanga ungeanza tuu ujenz wa nyumba yako!

Pia tambua wazaz na ndugu wanakutegemea usiongeze majukumu kwa kuwa una mafikirio yofauti. Hapo ni kwenu hakuna wakukusumbua kodi wala nn,kumbuka ukienda kuanza maisha mapya ya kupanga kuna kodi na gharama nyingine!

Na kama umefikiria kujitenga na ndugu zako uishi na mkeo basi usijenge hapo anzisha ujenzi wa hicho chumba kimoja unachokisema katika kiwanja chako.

Kumbuka kutowasahau wazee wako na ndugu zako ukifanikisha kuondoka hapo!

God bless u...!
 
Namba 3 hiyo inakufaa, save pesa yako malizia mjengo wako hamia mazima , maana hata baadhi ya ndugu zako utawasaidia kwa uhuru.

Kukaa hom na kufanya jambo kama hilo lako la kujenga ni kitu muhimu na hakuna kushangaana maisha ya town.
 
Kama una Mke bwashee... Tafuta nyumba ingine ya bei rahis... Tatizo lako unataka kukaa sinza na tabata. Nenda huko huko gomz ukiwa unajipanga kujenga. Afu badilisha hiyo ID, unajiita escobar kumbe bado unakaa home. Majina mengine yana mapepo hayo.
 
niungane na wote walio kushauri kwamba usijiingeze kwenye nyumba za kupanga.

Sijajua kwamba huyu mkeo mmesha oana au ndiyo mko kwenye mipango ya harusi.

Kama hamja funga ndoa basi ni vyema mkajipanga kwa muda mchache mkamalizia kwanza ujenzi wa nyumba yenu alafu ndiyo akaanza taratibu zingine.

Na kama ni mkewako tayari hunabudi kuishi nae hapo kwenu japo changa moto ni nyingi sana baina ya mama na mawifi zake yakupasa uwe na hekima sana kuishi na mkeo nyumbani kwenu.
 
Ndio ukubwa huo, fanya hivi usihame kwanza utajiongezea majukumu kwa kulipa kodi,

Na bado utatoa pesa ya matumiz kwako na kwa wazazi huoni itakua Ni ngharama?Ni bora mkae kwanza hapo hadi mtakapo kamilisha ujenzi wenu

hiyo room unayotaka kujenga kaijenge huko kwenye kiwanja chako ..

wazazi hawatapenda Sana kuondoka kwako kwa kuhofia kukosa msaada ,usije ukawasahau hata ukiondoka.

all the best
 
hasante sana kwa maoni yako, ndo maana huwa nawapenda wana JF kuwa mna mawazo mazuri
 
hasante sana kwa ushauri
 
hasante sana kwa maoni yako, ndo maana huwa nawapenda wana JF kuwa mna mawazo mazuri
Mkuu endelea kukaa nyumbani kwa malengo( kama walivyosema baadhi ya wadau hapo juu) huku ukijenga hata chumba kimoja kwenye kiwanja chako maana ukienda kupanga saiz gharama zitaongezeka pia hata wazazi na ndugu wataona kama umewatenga kuwakimbia ila ukijenga kisha ukahamia kwako moja kwa moja hayo yote yanaweza yasiwepo
 
hasante sana kwa mawazo yako mkuu
 
Kachimbe shimo la choo kwenye kiwanja chako(kama ni msimu wa mvua utapata maji ya kujengea hapo hapo), pandisha chumba kimoja(self) hamia kwako!!! Mengineyo mbele kwa mbele
 
Fanya yooote ila usiwatenge ndugu zako hasa wazazi et kisa unakwepa gharama....
unachopata hata km kidogo gawana na wazazi wako maisha yaendelee hasa kama wewe ndie pekee wanaekutegemea. Utabarikiwa machoni pao na machoni pa Mungu pia!!!!!!

Af zaid ya yote...nakushauri upunguze kucomplicate life, ishi uwezavyo...km unaenjoy kuwa na wazazi wako hapo home na unaamini nao pia wanafurahia uwepo wako na hasa msaada wako...kwanini uwakimbie bana! Nani kasema uanamume ni kuoa na kukaa mbali na wazazi???
 
ebwana hasante sana

ebwana hasante sana kwa mawazo yako, nashukuru sanaaaa
 
poa mkuu
Kachimbe shimo la choo kwenye kiwanja chako(kama ni msimu wa mvua utapata maji ya kujengea hapo hapo), pandisha chumba kimoja(self) hamia kwako!!! Mengineyo mbele kwa mbele
i respect your ideas, salute
 
Mkuu wewe endelea kukaa hapo home uanze ujenzi kwenye kiwanja chako mpaka utakapohamia ukipanga garam a itakuwa kubwa yapo mahitaji yatakoyo jitokeza zaidi....ukishahama chonde chonde chonde chonde usisahau baba mama na wadogo zako chonde chonde mkkuu
 
Hela ya kodi kajenge kwenye kiwanja chako
Hapo kwa wazazi wako waamzishie biashara wasikutegemee 100%
 
Back
Top Bottom