Msaada wa kazi jamani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msaada wa kazi jamani

Discussion in 'Nafasi za Kazi na Tenda' started by CPA, May 15, 2011.

 1. CPA

  CPA JF-Expert Member

  #1
  May 15, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 738
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 45
  Wana jf, nina dadayangu kamaliza degree ya sociology mwaka jana. Ametafuta kaz mpaka amechoka. Mwenye link ya kazi tafadhari anijulishe.
   
 2. Nanren

  Nanren JF-Expert Member

  #2
  May 15, 2011
  Joined: May 11, 2009
  Messages: 1,739
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Mwambie asitafute kazi Dar tu, pamoja na miji mikubwa. Halimashauri nyingi zina kazi. Ajaribu halimashauri za Tandahimba, Kishapu, Meatu, Simanjiro, Bukombe, Nanyumbu. Pia asisahau mikoa mipya ya Geita na Njombe/njoluma. Kazi atapata tu...
   
 3. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #3
  May 15, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280
  vijana wengi wanakosa kazi kwa sababu zifuatazo:
  1-wanachagua sehemu na aina ya kazi
  suluhisho:aombe kazi mahali popote tena zisizo na competition kubwa(mfano zikitangazwa posts za mtwara na dar aombe ya mtwara i.e. kama ni ofisi moja)

  2-Nt being agressive enough-wanafikiria ni nani anajuana na nani ili anisaidie.
  suluhisho: sometime tujifunze kumtegemea Mungu na akili zetu.awe bold enough to try anything

  3-Nt being creative-waajiri hawategemei kupata barua yako kuomba tu kazi,wanategemea kuona unasema utafanya nn kwa ajili yao ili kujazia kapu la kampuni na sio kuchota tu!
  suluhisho:muambie aangalie makampuni ambayo yako desperate kwa wafanyakazi (with turnover kubwa),aangalie interests zao.kisha aandike ''expression of interest letters'' akiomba either volunteering,internship ama ajira.hasa makampuni yaliyoko maporini kama ruvuma,geita,mtwara etc.
  kila la kheri kwake,hongera zake kwa kumaliza chuo.muambie tusiskie anaolewa hadi apate kazi,mwanamke kipato siku hizi

   
 4. A

  AridityIndex Senior Member

  #4
  May 16, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 121
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Miaka miwili mtaani hajaghairisha mpango wa kutafuta kuwa kibarua haaa.......tena na wewe unamsaidia kumfanya awe kibarua.

  Mwambie asitishe mpango mzima wa kutafuta kazi badala yake aje jukwaa la business akutane na akina millionea. Akiajiriwa atatupotezea ajira tunataka aajiri na azalishe ajira.
   
Loading...