Msaada wa Jina

Eng Kimox Kimokole

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2010
Posts
1,041
Reaction score
772
[h=5]Rafiki yangu (Muislam) anahitaji jina kwa kichanga chake cha siku moja kati ya majina haya;
1. Abraham,
2. Aaqil,
3. Munir

Lipi achague na kwa nini unadhani ulilochagua ni bora?
[/h]
 
Abraham....mtume wa Mwenye-enzi Mungu........hata baraka zitaambatana nae......jina pia huwa ni kiongozi wa maisha ya mtu......ajaribu kumuita Matatizo.....au Wasiwasi aone......
 
kwa siku ya leo jumatatu amuite abrahamu ingekuwa jumatano angemuita munir, hilo aaqil achana nalo, labda liwe wakil
niamini mimi....lakini ni bora ungesema na jina la baba ake tuone kama lina tamkikavizuri
 
Aaqil limekaa njema, nadhani linamaanisha Akili/upeo/welevu
 
Abraham....mtume wa Mwenye-enzi Mungu........hata baraka zitaambatana nae......jina pia huwa ni kiongozi wa maisha ya mtu......ajaribu kumuita Matatizo.....au Wasiwasi aone......

shukran Preta naendelea kupokea mawazo
 
Last edited by a moderator:
Rafiki yangu (Muislam) anahitaji jina kwa kichanga chake cha siku moja kati ya majina haya;
1. Abraham,
2. Aaqil,
3. Munir

Lipi achague na kwa nini unadhani ulilochagua ni bora?
Mkuu Kimox Kimokole Mwambie afanye hivi. ayaandike kwenye Vikaratasi 3 tofauti kila jina moja karatasi moja kisha avingirishe mzunguko wa duara halafu nenda na mtoto wako wa kike au wa kiume mdogo kiumri mwambiea achukue moja kati ya hyo majina matatu atakayo chukuwa ya kwanza ndio jina lake. Au Mwambie rafiki yangu Mzizimkavu ametoa jina linaloitwa (Muharram) Mwezi wa kwanza kwa kalenda ya kiislam ya mwaka mpya.fanya hivyo kisha uje hapa unipe fedback.
 
Hebu fikiria mtoto ukamwite Chausiku itakuwaje?
Mkuu.qKimox Kimokole Akimwita chausiku atakuwa ni Mwanga huyo Chausiku kiendacho usiku, au akimwita siwema au sikujuwa ,Au amwite Ubaya,Majina ya kizaramo hayo ee kasheshe majina yetu ya makabila ni upuuzi mtupu huo.
 
Tunafundishwa katika Uislamu kuwapa watoto majina mazuri. lakini majina sio yatakayo waingiza peponi. Mimi ni Muislamu lakini, sikusudii kumita mtoto wangu wowote kwa majina ya kigeni yoyote. Kwanini tusiwe kama Nigeria, japani etc. MAJINA YA KIARABU NA KIZUNGU NI UTUMWA TU, SIO DINI. HATA UKIITWA Juakali kibwengo, sawa tu. Ilimradi tu hilo jina liwe na maana.
 
Mkuu.qKimox Kimokole Akimwita chausiku atakuwa ni Mwanga huyo Chausiku kiendacho usiku, au akimwita siwema au sikujuwa ,Au amwite Ubaya,Majina ya kizaramo hayo ee kasheshe majina yetu ya makabila ni upuuzi mtupu huo.
Huu ni utumwa wa kiakili, si majina yote ya asili yetu yana Matatizo, imagine kama tutaukubali utumwa huu baada ya miaka 30 Tanzania nzima haitakuwa tena na Identification badala yake majina ni Juma, Jamal, Nassoro, Thomas, John Jimmy, huu ni upuuzi mtupu angalia Wazanzibar eti mtu Surname yake anaitwa Haji, Kombo, Juma. huku ni kutokujitambuwa.

Wakati wenzenu South Afrika wako bize baadhi ya miji barabara na viwanja vya ndege kuvibadili majina na kuita majini ya asili nyinyi mko bize kujikataa wenyewe.
 
Kweli vichwa vingine vinafuga nywele. MziziMkavu, stop that nonsense.
Mkuu Bigirita kwa majina ya kishenzi kweli nita stop that nonsense Siwezi kumwita Mwanangu et jina la

Siwema,Siwajuwi,chausiku,Cha kubimbi,Mwanauwani, na majina mengi mengineyo ya kipumbavu mimi ninayaaita

hayana faida unafikiri mwanaoukimwita mwizi na jee akiwa mkubwa akiwa jambazi utamlaumu nani? ukimwita sikujuwa

una maana gani hkujuwa kuwa Mungu atakupa mtoto? Upuuzi mtupu majina yetu ya kikabila ingawa mimi mwenyewe

Mzaramo na ni MziziMkavu Hauchimbwi Dawa.

Mkuu Matola Ujinga kwako wewe kwa watu wengine sio ujinga unamwita jina zuri lenye maana Mwanao si kumwita majina ya ovyo ovyo tu mkuu.

Mtu anayetumia muda wake mwingi kuangalia TV za Propaganda za Uarabuni unatalajia Ubongo wake usipige reverse?
Mimi sipo Uarabuni Mkuu Matola mimi jina langu si unalijuwa (MziziMkavu Hauchimbwi Dawa) Hilo jina langu la Kizaramo lakini ninapinga majina ya kikabila mengi yao hayo majina hayana maana chochote kile Siangalii TV Za Uarabuni mimi ninaangalia TV za ulaya Mkuu nipo Katikati ya ulaya sina time za kuangalia TV za Washenzi waaarabu mkuu.
 
Last edited by a moderator:
Rafiki yangu (Muislam) anahitaji jina kwa kichanga chake cha siku moja kati ya majina haya;
1. Abraham,
2. Aaqil,
3. Munir

Lipi achague na kwa nini unadhani ulilochagua ni bora?

Baba mtoto anaitwaje? naomba kujua hili ili nijui ku-combine !!
 
Kuna jirani yangu hapa anawatoto watatu na majina yao kama ifuatavyo;
1)HAWA
2)HATUFIKI
3)MWATAKAJE

So you may choose one of them!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…