Msaada wa haraka wa chuo na course

omoghaka

JF-Expert Member
Dec 21, 2012
293
166
Naomba kwa yeyote mwenye uelewa anisaidie kunifahamisha chuo kizuri kilichopo DSM au Nje ya DSM ambapo naweza kumpeleka mwanangu akasome Kozi itakayomsaidia.Kamaliza Kidato cha Nne 2016 na Kupata Division Four Points.27 kama ifuatavyo:

KISWAHILI C

ENGLISH C

GEOGRAPHY D

HISTORY D

BIOLOGY D

CIVICS D

B/MATHS F

B/KEEPING F

COMMERCE F

Naombeni msaada wenu maana nasikia vyuo vinaanza kutoa Application Forms hivi karibuni.
 
Google chuo cha serikali za mitaa hombolo ni kizuri Mimi pia Nitampeleka mdogo Wangu...!!
 
Ila unaweza kumpeleka sheria, sociology, au mambo ya ustawi,
Vyuo ni ustawi, tumaini, mwl. Nyerere, magogoni
 
Nashukuru lakini nahisi upatikanaji wa Kazi baada ya Masomo ni mgumu.
Hapana Hicho chuo Ndo Kinatoa wataalamu wengi WA tamisemi na mashirika mbalimbali angalia kozi zipo nyingi nzuri
Au kwa dsm mpeleke DiT
Mbeya mpeleke MuSt google hivyo vyuo ni vizuri vya Serikali..
Kwa ufaulu wake tena wa biology Anaweza somea masuala ya vyakula au laboratory technician
Asante
 
Wasiwasi wangu ni kwamba Kapata F ya B/Mathematics hivyo ni vigumu kupata nafasi ya kusoma MuST na DIT.
 
DIT na MUST short course au??
Ni chuo gan kigezo cha kusoma lab tech na food science ni D ya biology?
 
VYUO VIPO VINGI DAR ANAVYOWEZA KUSOMA ILA UNACHOTAKIWA KUJIULIZA NI KOZI IPI BORA AKISOMA ITAYOMUWEZESHA KUPATA AJIRA KWA URAISI............

MIMI KATIKA UTAFITI WANGU COURSE AMBAZO ZINATOA AJIRA KWA. HARAKA NI TANO.

1.UALIMU WA CHEKECHEA.

2.ELECTRICAL FENCE AND CCTV SYSTEM

3.CHINNISE LANGUAGE

4.PAINTING AND DECORATIONS.

5.GRAPHICS DESIGNER

NA VYUO MPELEKE D.I.T , VETA, UCC LAKINI

UKISEMA UMPELEKE CBE,IFM,ITA,TIA,KIU, UDSM,TUMAINI HUKO KUSOMA ATASOMA ILA ITAMCHUKUA MUDA MREFU KUPATA KAZI KWA SABABU HIVYO VYUO FANI ZAO ZIMEJAA KATIKA SOKO LA AJIRA
 
Mpeleke Don Bosco Oysterbay akasomee carpentry au Electrical Installation,,,ajira njenje na pia kile chuo kina tabia ya kutafutia wanafunzi ajira au kuwaajiri kwenye karakana zao
 
Wasiwasi wangu ni kwamba Kapata F ya B/Mathematics hivyo ni vigumu kupata nafasi ya kusoma MuST na DIT.
Ni hivi DiT muhula wa masomo huwa unaanza mwezi wa 10, Lakini yeye atasoma wiki 10 kuanzia mwezi wa 7 ili Aje aanze masomo na Wenzake mwezi wa 10
Kingine Ndg ingia mtandaoni utaona info zote unazohitaji kujua na namba za kuwasiliana nao wala usipate wasiwasi Ndg
 
VYUO VIPO VINGI DAR ANAVYOWEZA KUSOMA ILA UNACHOTAKIWA KUJIULIZA NI KOZI IPI BORA AKISOMA ITAYOMUWEZESHA KUPATA AJIRA KWA URAISI............

MIMI KATIKA UTAFITI WANGU COURSE AMBAZO ZINATOA AJIRA KWA. HARAKA NI TANO.

1.UALIMU WA CHEKECHEA.

2.ELECTRICAL FENCE AND CCTV SYSTEM

3.CHINNISE LANGUAGE

4.PAINTING AND DECORATIONS.

5.GRAPHICS DESIGNER

NA VYUO MPELEKE D.I.T , VETA, UCC LAKINI

UKISEMA UMPELEKE CBE,IFM,ITA,TIA,KIU, UDSM,TUMAINI HUKO KUSOMA ATASOMA ILA ITAMCHUKUA MUDA MREFU KUPATA KAZI KWA SABABU HIVYO VYUO FANI ZAO ZIMEJAA KATIKA SOKO LA AJIRA

Nimekuelewa vizuri.Naomba unifahamishe hiyo CHINESE LANGUAGE na ELECTRICAL FENCE AND CCTV SYSTEM inafundishwa wapi?
 
Ni hivi DiT muhula wa masomo huwa unaanza mwezi wa 10, Lakini yeye atasoma wiki 10 kuanzia mwezi wa 7 ili Aje aanze masomo na Wenzake mwezi wa 10
Kingine Ndg ingia mtandaoni utaona info zote unazohitaji kujua na namba za kuwasiliana nao wala usipate wasiwasi Ndg
Mkuu mbona unapotosha waziwazi
DIT na MUST pre entry lazima mtu awe na D kwenye Physics,Chemistry,B/math na English/Biology
huyo kwanza ana F ya hesabu pili hajasoma sayansi
Hawezi sio tu kwenda ata ku apply DIT
 
Nimejaribu kuscreenshort hazipo katika mpangilio mzuri Lakini zitakusaidia...!!
d2c7dc909dd3c3f6345804b44f9a55c6.jpg
c6983a79c6e8f4d5a04679d63b2036e5.jpg
c47740b9f3fba52c578d1b2e98789193.jpg
9018973f9594f55a3316f26a1e6505f0.jpg
af8b8bd1cc80692c506ee4bfac76bfe0.jpg
b3651bc3d42698767eeca760cff583a9.jpg
 
Back
Top Bottom