Msaada wa haraka unahijitajika tafadhali wana- JF

m.agape

Senior Member
Joined
Dec 7, 2012
Posts
149
Reaction score
94
Nina Diploma ya Biashara ambayo niliipata mwaka 2010 katika chuo cha Uhasibu Tanzania( T.I.A). Toka muda huo sijawahi kupata ajira.

Ni mwanadada umri miaka 26. Nimekuwa nikiuza duka na kufanya huduma zote kama muuzaji, mtunza kumbukumbu za mauzo bidhaa pamoja na pesa. Pia ninafanya mahesabu ya vikundi vya kina mama mtaani kwetu.

Kwa sasa sina kipato chochote.na nimeelemewa na majukumu. Baada ya kufariki baba yangu, nimeachiwa jukumu la kutunza familia na kuendeleza wadogo zangu kielimu.

Naombeni msaada nipate kazi yoyote hata kibarua niko tayari.

Ninaishi kawe maeneo ya Kawe Bondeni.

Natumai ombi langu litashughulikiwa.
Nawatakia kazi njema.
 
kwanini unafikilia kuajiriwa tu badala ya kujiajiri..
 
Napenda sana kujiajiri na wazo hilo ninalo, tatizo mtaji ndugu.
 
Pole sana dada! Nakushauri usikate tamaa, pia usisubirie mpaka nafasi zitangazwe kwenye ofisi husika ndiyo uapply.Kuwa unatembelea ofisi ambazo unadhani una-qualify kufanyakazi hasa ofisi za binafsi! Don't give up, keep on fighting. Mungu akufanyie wepesi kwenye mambo yako.
 
Nina Diploma ya Biashara ambayo niliipata mwaka 2010 katika chuo cha Uhasibu Tanzania( T.I.A). Toka muda huo sijawahi kupata ajira.

Ni mwanadada umri miaka 26. Nimekuwa nikiuza duka na kufanya huduma zote kama muuzaji, mtunza kumbukumbu za mauzo bidhaa pamoja na pesa. Pia ninafanya mahesabu ya vikundi vya kina mama mtaani kwetu.

Kwa sasa sina kipato chochote.na nimeelemewa na majukumu. Baada ya kufariki baba yangu, nimeachiwa jukumu la kutunza familia na kuendeleza wadogo zangu kielimu.

Naombeni msaada nipate kazi yoyote hata kibarua niko tayari.

Ninaishi kawe maeneo ya Kawe Bondeni.

Natumai ombi langu litashughulikiwa.
Nawatakia kazi njema.

mi umenichanganya hapo kwa red!
 
Pole sana dada! Nakushauri usikate tamaa, pia usisubirie mpaka nafasi zitangazwe kwenye ofisi husika ndiyo uapply.Kuwa unatembelea ofisi ambazo unadhani una-qualify kufanyakazi hasa ofisi za binafsi! Don't give up, keep on fighting. Mungu akufanyie wepesi kwenye mambo yako.
asante sana kwa ushauri wako. Nimezunguka kila ofisi bila mafanikio.
 
mi umenichanganya hapo kwa red!

kuna boss alinikabidhi duka lake, nisimamie na kufanya kazi zote zinazohusiana na maduka, halafu mwisho wa mwezi tunagawana kilichopatikana.tulifany biashara vizuri kwa kweli. Baada ya kurudi msiban boss akawa amekatisha mkataba.

Kuhusu mahesabu, kuna vikundi vya kina mama mtaani wananunua hisa na kukopeshana kila baada ya miezi 6 wanagawana. Hapo ndio wananiletea niwapigie hesabu, wajue nani anadaiwa na faida iliyopatikana.

Natumai umenipata vizuri.
 
inawezekana njia ulizotumia hazikua sahihi kutafuta kazi sehemu ambayo hujui kama wanaitaji m2 au la sasa fanya hv nenda kwenye library yoyote maktaba au tanganyika na nk uwe unasoma magazeti mbalimbali kwa ajili ya kazi jiandikshe hapo uwe member na uwe unaenda mara 1 kwa wik upitie magazeti yote ya wik hapo utafanikiwa
kuna vacancy nying sana huku sema wabongn weng hawapend kusoma
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom