Fadhili Paulo
JF-Expert Member
- Sep 1, 2011
- 3,211
- 996
Kakope sehemu ingine umlipe kuepuka mlundikano wa riba (lipa deni kwa kutumia deni jipya)
Ndiyo mkuu ndiyo biashara yake ila hana leseni na hata kama angekuwa na leseni sidhani kama angeruhusiwa na vyombo husika.Riba ya 50% kwa mwezi? Huu ni wizi wa mchana! Huyo jamaa ndio biashara yake? Ana leseni ya kufanya hiyo bishara?
Mkuu, nashukuru kwa ushauri wako ila suala la kwenda kukopa kwingine hilo ndilo gumu sitaki kabisa kusikia tena mambo kama haya ni bora anipeleke polisi.Kakope sehemu ingine umlipe kuepuka mlundikano wa riba (lipa deni kwa kutumia deni jipya)
Kweli kakope kwingine Laki mbili na nusu jazia na hiyo laki mbili mpelekee 450,000/= hao watu sio wazuri maana akiikamata hiyo hela atakata riba 150,000/= akuache na 50,000/=
Hata mahakamani utapewa muda kama unazo kidogo lakini ukigoma kumlipa hata senti siku hizi wanawekwa jela na kulipiwa malazi na chakula ukitoka unalipa vyote deni na chakula/ malazi uliyoyatumikia
Mpelekee 450,000/= mbele ya Mdhamini au shahidi au Balozi
Kumbuka kuwa kisheria haitakiwi Malipo ya deni na. riba kuzidi kiasi kilichokopwa. Hii inaitwa duplum principle. Wale mashylocke wanaoishi kwa riba za mikopo hawataipenda hii lakini that's the fact.
Mkuu, nashukuru kwa ushauri wako ila suala la kwenda kukopa kwingine hilo ndilo gumu sitaki kabisa kusikia tena mambo kama haya ni bora anipeleke polisi.
Hawezi kukufunga hiyo ni kesi ya madai, muache akudai akikupeleka mahakani kesi inaisha mwaka 2020 hadi raha