Msaada wa haraka kuhusu kupata TIN number ya kampuni na kufungua account ya kampuni bank

Tokez

Member
Oct 4, 2012
68
22
Habari za weekend!

Nina kampuni yangu nimefungua tangu mwaka 2017 lakini nilishindwa kumalizia process za kupata TIN NO. na leseni ya biashara so naomba msaada kwa anayefahamu ni vitu gani vinahitajika ili kukamilisha zoezi hili?
Aina ya kampuni ni limited na tupo directors wawili ila jamaa yangu yupo mbali now so nipo mwenyewe na nataka kukamilisha usajili kwa ridhaa yake.

Pia namna ya kufungua account ya bank ni vitu gani vitahitajika niviandae ili mungu akipenda kesho nianze mchakato wa kufungua account ya kampuni?

Bank niliyokusudia kufungua ni NMB ndio naona itanirahisishia mambo yangu yote.

Natanguliza shukrani kwa msaada mtakaonipa.
 
Kwa TIN number tumia online portal ya TRA utajaza kupitia namba yako ya NIDA
 
Naona private text zinagoma kuja kwako sijui tatizo nn
Nenda tra na memart ya kampuni yako, mkataba wa kodi ya pango, copy za id za wakurugenzi wote wa kampuni na mwisho kabisa copy ya cheti cha usajili wa kampuni hapo tin umepata
 
Na kuhusu kufungua account ya kampuni unatakiwa uwe na tin no ya kampuni, cheti cha usajil wa kampuni,leseni ya biashara iliyo active, copy za vitambulisho kwa watia saini paspot size mbili kila mmoja, barua kutoka kwenye bodi ya wakurugenzi kuonyesha jinsi mtakavyo irun hiyo account na pia barua ya kuomba kufungua account ya bank kutoka kwenye bodi ya wakurugenzi wa kampuni
 
Umetiririka maridadi kabisa mkuu

Back
Top Bottom