Msaada wa haraka: Chuo cha mipango dodoma vs chuo cha utumishi

Msaada wa haraka: Chuo cha mipango dodoma vs chuo cha utumishi

kiongozirorya

Member
Joined
Jun 23, 2013
Posts
5
Reaction score
1
WANAJAMVI,
Kwanza naomba msamaha kwa kuandika habari hii kwenye hili jukwaa badala ya jukwaa la Elimu. Sababu kubwa ni kwamba, hili jukwaa lina watu wengi sana, na mimi nahitaji ushauri wa haraka sana katika hili.

Mimi ni muhitimu wa Form 4 mwaka jana. Matokeo yangu hayakuwa mazuri sana, hivyo niliomba kusoma Certificate kwenye Chuo cha Utumishi Tanga kusomea Local Government Administration, na Chuo cha Mipango Dodoma kusomea mambo ya mipango. Na kwa bahati nzuri, kote nimechaguliwa. Sasa naomba ndugu zangu watanzania mnishauri ni chuo gani nikasome? Vigezo vya ushauri vizingatie;

1. Course gani ina soko katika mambo ya ajira iwe serikalini au kwenye taasisi za watu binafsi.

2. Course gani ina manufaa mapana kuliko nyingine

3. N.K.

Ahsanteni sana na ninatanguliza shukrani.
 
Mmmmmmhhhhhh, cjuw cha kuandika! But coz hizi zote ni bahati tu kupata kazi!
 
Nimesoma mipango, nakushauri ukasome mipango course hiyo certificate in rural planning (CRP) kwa sababu wewe mwenyewe ukitoka pale utaweza kupanga maisha yako ya baadae, pia wanakwenda mafunzo kwa vitendo mkiwa katikati ya masomo ambapo hakuna chuo chochote kinafanya hii maneno ya field kiongozirorya
 
Last edited by a moderator:
Ila kama ni lelemama na sio mtu wa kusoma na kuelewa, pia hesabu kama mama mkwe kwako Mipango sio mahali pako. Kwa sababu kila course pale ina hesabu na uchumi kiongozirorya
 
Last edited by a moderator:
haya ndio matatizo ya wanavyuo wengi unataka kuanza chuo na hujui unataka kusomea jambo gani,sasa sisi wanajamvi tukushauri vipi wakati wewe haujitambui?

Jambo la kwanza jitazame unachotaka kusoma then watu ndio uje uombe ushauri.
 
Ahsante kwa maoni yako. Ungekuwa na uelewa mzuri ungeweza kuelewa ni kwanini niliomba hivyo vyuo tena katika ngazi ya cheti. Siyo siku zote kila mtu anapata kile anachohitaji. Wakati mwingine mazingira yanakusukuma kuchukua maamuzi fulani japo hukupanga toka mwanzo. Na inapotokea hivyo, basi siyo mbaya kuomba ushauri kwa watu wengine wenye uelewa katika mambo hayo. Hata mimi mazingira (matokeo yangu ya form 4) ndiyo yalisababisha nikaangukia huko. Na kwasababu nimepata nafasi zote mbili, ndiyo maana nimekuja kwa watanzania wenzangu wenye kuelewa nini maana ya mtu kuomba ushauri ili wanisaidie ushauri, ili baada ya kuangalia ushauri wao, ndipo na mimi niamue ni course gani nikasome.

Hatahivyo, nashukuru kwasababu tuko tofauti na hata mawazo yetu yako tofauti.

NB: Jamani nawaomba muendelee kunishauri, kwani nahitaji nijipime na kufanya maamuzi ni chuo gani niende.
 
WANAJAMVI,
Kwanza naomba msamaha kwa kuandika habari hii kwenye hili jukwaa badala ya jukwaa la Elimu. Sababu kubwa ni kwamba, hili jukwaa lina watu wengi sana, na mimi nahitaji ushauri wa haraka sana katika hili.

Mimi ni muhitimu wa Form 4 mwaka jana. Matokeo yangu hayakuwa mazuri sana, hivyo niliomba kusoma Certificate kwenye Chuo cha Utumishi Tanga kusomea Local Government Administration, na Chuo cha Mipango Dodoma kusomea mambo ya mipango. Na kwa bahati nzuri, kote nimechaguliwa. Sasa naomba ndugu zangu watanzania mnishauri ni chuo gani nikasome? Vigezo vya ushauri vizingatie;

1. Course gani ina soko katika mambo ya ajira iwe serikalini au kwenye taasisi za watu binafsi.

2. Course gani ina manufaa mapana kuliko nyingine

3. N.K.

Ahsanteni sana na ninatanguliza shukrani.

Kwa nini uwaze kuajiriwa badala ya kujiajiri?
 
Back
Top Bottom