Msaada Wa Ajira Portal "Application FAILED"

AgentX

JF-Expert Member
Mar 7, 2015
1,650
1,687
Habari Wakuu poleni na majukumu.

Naombeni Msaada Tutani Wakuu.
Mwishoni kabisa mwaka Jana niliamua kufungua akaunti ya ajira portal na Mimi ili nikiona kazi niombe Ila Kuna changamoto so unajua Tena Hawa IT wa serikalini kazi yao ni kudownload movie tu na si kuboresha kinachowapatia ugali
Nikiri kabisa nimekuwa nikiona malamiko mengi mno humu ndani kuhusu huu mtandao wetu pendwa.
Moja kwa moja niende ktk mada
Nilikuwa naomba kazi ambayo nadhani vigezo ninavyo Ila nakutana na ujumbe wa "application failed" pale tu ninapobinya "apply" kwa wajuzi naomba mniambie nakosea wapi.

Profile Dashboard inaniambia nimekamilisha taarifa kwa 95% je hizi hazitoshi Hadi ifike 100%? Naombeni mnieleze Wakuu

Pili, sehemu waliyoweka Declaration inatakiwa u- tick (check) lakini kwangu sipati iyo option kwani iko "greyed out" Sasa sijui Nakosea wapi Wakuu

Tatu ndo hivyo Tena akaunti ninayo nashindwa ku apply

Attachments below
View attachment 2533429View attachment 2533430View attachment 2533431
 
Attachments

  • Screenshot_20230301-093625_1677652709963.jpg
    Screenshot_20230301-093625_1677652709963.jpg
    44.5 KB · Views: 70
Huko kama wanataka mtu mwenye diploma na profile yako inasema una degree mzee lazima igome.

Umezungatia hilo?
Mi ni dereva. Nilieka Cha VETA tu, leseni na Cha O level Sasa mambo yangu ya DIT sijaweka kabisa coz cheti sikuwa nacho by then nafungua akaunti kozi Hawa ajira portal unajaza elimu huku unambatanisha na cheti as PDF.

Ila ipo siku niliomba nafasi ya udereva ilinigomea hivyo hivyo .

Instincts zangu zinaniambia hapa ktk "declaration" ndo Natakiwa ni "check" Ina maana Kama nimedondoka signature Ila changamoto ni kuko greyed out yaani hakushikiki wakati ilitakiwa no press "check" then ni save Ila inanigomea.

Nafasi Yenyewe niliyokuwa naomba ni ya kawaida Sana
Attachments below mkuu
Screenshot_20230301-093625_1677652709963.jpg
View attachment 2533470
 
MKUU cheti ni Cha VETA tu nilieka. Tena Cha Basic Driving na form four Basi tu. Valid license na other data Ila ktk academic ni hizo tu .... Sikutaka niwwke mavyeti Mengine
Screenshot_20230301-100425.jpg
 
Sasa hapo unatakiwa uweke cheti cha form four na form six na hiyo leseni tu, hawataki korokoro zingine ndio maana inakugomea kama umeweka na mbwembwe zingine

Sent from my Infinix PR652B using JamiiForums mobile app
 
Hiyo post anayoizungumzia inataka mtu wa form four na mwenye leseni ya kuendesha pikipiki kwa mujibu wa sifa zilizoainishhwa katika tangazo.
 
Kwa ushauri wangu kama upo dar nenda leo ofisini kwao wakurekebishie hiyo akaunti yako Bila hivo deadline kesho na hutaiwahi, pole kwa maswahibu yote hayo

Sent from my Infinix PR652B using JamiiForums mobile app
 
Cheti Cha VETA kinakaa ktk Training and Workshop au Academic Qualifications?

Manake leseni iko sehemu sahihi ktk Professional Qualifications!

Na kwanini hawajaeka option ya kufuta mtu mwenywe mbona Kama ilivyokuwa KUJAZA SI NI MIMI MWENYWE?

HII NCHI URASIMU UTAISHA LINI?

LESENI YANGU NAENDESHA PIKIPIKI MPAKA LORI WHY IGOME?
WTF?
 
Na vipi kuhusu hii Declaration ndo Hamna mwenywe majibu?
 
Na vipi kuhusu hii Declaration ndo Hamna mwenywe majibu?
Hiyo Declaration yako inaonekana umeshapiga tick hapo nyuma. Ni swala la kukumbuka. Maana ikiwa bado huwa ipo fainted bila Alama ya tick kuonekana kwenye Kibox.
 
Cheti Cha VETA kinakaa ktk Training and Workshop au Academic Qualifications?

Manake leseni iko sehemu sahihi ktk Professional Qualifications!

Na kwanini hawajaeka option ya kufuta mtu mwenywe mbona Kama ilivyokuwa KUJAZA SI NI MIMI MWENYWE?

HII NCHI URASIMU UTAISHA LINI?

LESENI YANGU NAENDESHA PIKIPIKI MPAKA LORI WHY IGOME?
WTF?
Yaani binadamu bwana, umepata changamoto kidogo unaanza kulaumu kuwa urasimu ni mwingi. Jaribu kuwa na mtazamo chanya uta enjoy maisha. Wame avoid kufuta mwenyewe kwa sababu mtu anaweza ona tangazo la diploma na yeye ana diploma na degree akaamua kufuta degree ili aombe kazi
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom