Msaada utaalamu wa kufuga Bata bukini

kumbwitu

Member
Apr 11, 2017
19
45
Poleni na pilika za ujenzi wa taifa,naomba kwa anayefahamu jinsi ya kuwafuga Bata bukini,nilinunua Bata wawili jike na dume toka mwaka Jana mwezi wa Tisa lakini chaajabu mpaka leo hawajaanza kutaga .sijajua nimekosea wapi ,naomba msaada wa elimu namna ya kuwafuga ili waweze kuleta tija
 
meme

Member
Aug 12, 2013
37
95
Wajengee kisima na wape sana majani ndio Chakula chao utaona matokeo
 
fundi25

JF-Expert Member
Apr 16, 2013
8,112
2,000
Mkuu isije kuwa unafuga madume yote pia hao ndege ni wagumu sana kutaga !!
Poa alichokuambia meme kama huwapi majani mengi utakuwa unawatesa wanakula majani kwa 60% ya chakula kingine wanatakiwa wawe wana kunya kinyesi cha rangi ya majani tupu kama ngombe!!
 
Kishalu

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
1,174
2,000
Lazima wapate sehemu ya kuoga siku zote na maji yawe yanabadilishwa na wape chakula cha kutosha mara nyingi huwa ili awe fertile anakuwa kwenye maji na dume.Chakula ni kawaida kama Bata mzinga tu
 
mamseri

JF-Expert Member
Oct 5, 2012
685
250
Pia hutaga Mara moja kwa mwaka Ila ndio msimu wao sasa hiv mpaka mwezi was nane

Sent from my TECNO-C8 using JamiiForums mobile app
 
AsiliYetu

Member
Jun 3, 2016
62
95
Mimi nafuga niliwanunua mwaka jana Saba saba wakataga na kutotoa vizuri lakini sasa hivi wamelalia wa wili wote mayai yamehalibika. ukiyavunja ndani yanatoka maji meusi na harufu kali sana

Sent from my E6633 using JamiiForums mobile app
 
fundi25

JF-Expert Member
Apr 16, 2013
8,112
2,000
Kubwa moja na madogo matatu

Sent from my E6633 using JamiiForums mobile app
Mkuu nilipatwa na tatizo kama hilo mara ya kwanza waliangua baada ya kuwafuga kwa miezi 6 aliangua vifaranga wote kabla zija wajengea kisima ila madume nilikuwa nao watano nilichogundua hawa ndege huwa dume moja huwa kiongozi na lazima atakuwa mtata sana huwa harusu mwingine kupanda hata kama yeye ni dume suruali huwa linakuwa na mkwara sana kwa madume mengine na madume mengine humuheshimu sana !!
Chunguza utaona ata kutangulia mbele lazima litanguliye hilo babe kwanza likitembea kila dakika fulani huangalia kama kuna dume linatongoza mkuu huyu hawa ndege siyo kama jogoo huwa yana chukua kama dakika 3au 4 adi lipande juu ya jike sasa hapo dume hawezi panda maana yana wivu sana na huwa madume mengine yote lazima yanapokea muongozo kutoka kwa huyo mbabe
note hawa jamaa wakiwa kwenye maji hawanaga nguvu kabisa ya kupandana ni mara chache sana na ni tukio la bahati nasibu kupandana ndani ya maji !!
Ondoa huyu dume anaye anayepita mbele na kupiga kelele siyo mpandaji!!
 
Kiberiti Kidogo

JF-Expert Member
Jan 14, 2017
576
1,000

Sorry sijakusomq fresh. Inamaana ukitaga kufuga linatakiwa dume moja?
 
fundi25

JF-Expert Member
Apr 16, 2013
8,112
2,000
Sorry sijakusomq fresh. Inamaana ukitaga kufuga linatakiwa dume moja?
Nilicho jifunza kwa hawa jamaa kwa kukaa nao mda mrefu unaweza ukawa una madume 3majike 6 na yote yasitage mayai yenye mbegu maana kwenye hayo madume 3 kuna moja litakuwa tata sana likimuona dume anaye taka kupanda anakuwa adui yake mkubwa sana hawataelewana na tabia ya hilo dume tata huwa halipandi unaweza kuwa na madume matatu yote yakawa mapole !!
Me nilifuatilia kwa mda sna mkuu na kila miezi inapoongezeka dume wa aina hiyo huongezeka ubabe anaweza kukurukia ata wewe mwenyewe mfugaji!!!
Lina kazi moja tu kutawala mengine na kizuwia mengine yasipande chunguza kama una wafunga na hawaangui utaone hicho ninacho kuambia!
 
kawombe

JF-Expert Member
Mar 26, 2015
4,064
2,000
Kweli Ndg ? Wapi huko bata wanapouzika aiseeh ?

Sent from my HUAWEI Y336-U02 using JamiiForums mobile app
Saba saba au kama upo DAR ni pale kijiji cha makumbusho. Pia kuna jamaa wanaitwa NKUZA wako karibu kabisa na KIBO COMPLEX TEGETA KIBAONI. unawapata pale
 
shivo01

Member
Mar 25, 2014
89
150
Mimi nafuga niliwanunua mwaka jana Saba saba wakataga na kutotoa vizuri lakini sasa hivi wamelalia wa wili wote mayai yamehalibika. ukiyavunja ndani yanatoka maji meusi na harufu kali sana

Sent from my E6633 using JamiiForums mobile app
Hao ndo tatizo lao huwa wanataga mara moja kwa mwaka na kwenye kulalia wanalalia wote kwa pamoja na kuharibu mayai,me baada ya kugundua hivyo huwa nawatenganisha vibanda
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom