Mkuu nilipatwa na tatizo kama hilo mara ya kwanza waliangua baada ya kuwafuga kwa miezi 6 aliangua vifaranga wote kabla zija wajengea kisima ila madume nilikuwa nao watano nilichogundua hawa ndege huwa dume moja huwa kiongozi na lazima atakuwa mtata sana huwa harusu mwingine kupanda hata kama yeye ni dume suruali huwa linakuwa na mkwara sana kwa madume mengine na madume mengine humuheshimu sana !!
Chunguza utaona ata kutangulia mbele lazima litanguliye hilo babe kwanza likitembea kila dakika fulani huangalia kama kuna dume linatongoza mkuu huyu hawa ndege siyo kama jogoo huwa yana chukua kama dakika 3au 4 adi lipande juu ya jike sasa hapo dume hawezi panda maana yana wivu sana na huwa madume mengine yote lazima yanapokea muongozo kutoka kwa huyo mbabe
note hawa jamaa wakiwa kwenye maji hawanaga nguvu kabisa ya kupandana ni mara chache sana na ni tukio la bahati nasibu kupandana ndani ya maji !!
Ondoa huyu dume anaye anayepita mbele na kupiga kelele siyo mpandaji!!