Msaada: ushauri wa kitaalam Maumivu Ya Mfumo Wa Faham

Majigo

JF-Expert Member
Feb 23, 2012
5,519
1,825
Usichoke kusoma tafadhari

Ni mda wa miaka mitano sasa siko sawa ,kichwani hadi mapajani napata maumivu yasiyo ya kawaida, misuli inakaza, mishipa inauma, napata uchovu kiasi nalala mara kwa mara, nashindwa kufikiri kwa upana kwani nahisi uchovu wa akili na mwili.
Angalau Napata nafuu kidogo sana nikifanya mazoezi Asubuhi .

Nilikwenda mnazi mmoja hospital nikafanya full blood chaking na mkojo ila hawakuona kitu zaidi ya UTI ,Nilipewa dozi Nikamaliza lakini hali ile haikuisha hata kidogo

Kuna mahali nilisoma kuhusu nerve pain nikajaribu dozi ya NEUROTONE nilipata nafuu ila baada ya kumaliza dozi hali ikarudi kama mwanzo

Najinyoosha maungo yangu mara kwa mara na nahisi ile sauti ya kunyoosha msuli uliopinda hasa mgongoni hadi kichwani

Nisaidieni Wakuu kwani nahisi kabisa siko sawa kama wenzangu!
 
Back
Top Bottom