Msaada: Nasumbuliwa na maumivu makali ya kiuno kila nikikaa au nikisimama

toplemon

JF-Expert Member
Mar 26, 2017
4,581
4,631
Ni mwezi wa pili sasa nasumbuliwa na matatizo ya kiuno kila nikisimama au nikikaa muda mrefu

Nikikaa chini kuja kunyanyuka napata maumivu makali sana kuna wakati kiuno kilikamata hadi nasimama kwa kutumia vitu

Kutembea natembea vizuri ila nikijaribu kuimana kuinuka kuna sehemu ya kushoto inauma balaa

Mwanzo nilihisi ni U.T.I nikameza dozi za kutosha za u.t.i bila kupata nafuu

Niliamua kwenda hosptali nikapimwa damu na magonjwa ya zinaa yote hadi ukimwi, malaria nk.....

Matokeo ya vipimo ilionekana sina STD's wala sina malaria wala homa walikuta nina u.t.i ila kidogo sana

Nikapewa dawa nikameza, nikamaliza nikarudi kuchukua nyingine lakini wapi japo nilipata kaunafuu but kiuno bado kinanisumbua sana

Nishaurini wakuu jee nitumie tiba au dawa gani nipone??
 
Pole sana top lemon.
Check hospital nyingine siunajua doctors unaweza ikawa unafanyiwa practical bila kujua.
Ukafanye vipimo zaidi
 
Lumbar Vertebrae kati ya L1 mpaka L5 ndio zina shida bila shaka, nenda hospital nyingne kwa uchunguzi zaidi, pia anza kujichua.
 
Hapo usichelewe wala kuanza kusikiliza ya wananzengo nenda hospitali lipia fanya vipimo wakutizame nn kinasumbua kati ya kiuno au uti wa mgongo usifanye mchezo kabisa wala usipoteze muda ili kama ni matibabu yaanze mapema

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
it’s more likely spondylosis , you need lumber sacral x ray to verify the diagnosis for now you need anti pain then physiotherapy with minimal weight bearing activities and lose that weight
 
Lumbar Vertebrae kati ya L1 mpaka L5 ndio zina shida bila shaka, nenda hospital nyingne kwa uchunguzi zaidi, pia anza kujichua.
Probably itakuwa hiyo.
I experienced such situation, nikaenda kupima kwa wakati ule kwa CT Scan. Majibu yalikuwa kama ulivyosema mkuu. Nilianzishiwa mazoezi nikapata nafuu sana. Mazoezi yake si mchezo. Wale watu wa mazoezi, wee acha tu. Hata hivyo nawashukuru sana.

Awahi mazoezi mapema. Pia atapata ushauri muhimu toka kwa wataalamu/madaktari wenye profession yao.
 
Asante sana
 
it’s more likely spondylosis , you need lumber sacral x ray to verify the diagnosis for now you need anti pain then physiotherapy with minimal weight bearing activities and lose that weight
Shukran sana
 
Tafuta dawa inaitwa KIPASI inapatikana kwenye maduka ya dawa za asili, bei yake ni kati ya TSH. 8000/ ~ 10000/ ilinisaidia sana wakati nimesumbuliwa na tatizo kama ulilowleza.

Wakati huo huo uendelee kuhudhuria hospital kupata ufumbuzi wa nini kinakusumbua.

NB; hiyo dawa ni ya kuchua sehemu panapokusumbua
 
Back
Top Bottom