Salaam nyote wanajukwaa. Poleni na hongereni kwa juhudi zote mzichukuazo dhidi ya janga hatari la corona.
Naomba niende kwenye mada moja kwa moja.
Mimi muhitimu wa shahada ya sayansi elimu (bsc ed, masomo yakiwa Physics & Biology) kwa sasa ni mtumishi wa umma, idara ya elimu yaani mwalimu, na mwaka moja na miezi 6 sasa tangu niajiriwe.
Sasa nimefikiria kusoma masters ya kozi kadhaa ambazo naomba kwa mwenye ufahamu aniongezee kama ni bora kwa soko la ajira la Tanzania, lengo kuu hasa la kusoma masters ni kuja kua LECTURER (bsc ed gpa ni 3.9) au kupata kazi yenye maslahi zaid kwenye MASHIRIKA MAKUBWA duniani kama Save the children, Norwegian refugee council (NRC) na nakadhalika.
Kozi nilizozifikiria hizi hapa;
1. Masters in Public health chuo ni MUHAS
2. Masters of science in Biochemistry chuo ni MUHAS/UDSM/SUA
3. masters of science in Physics chuo ni. UDSM (japo si mzuri sana kwenye mathematics, hasa advanced mathematics nadhani nitatoboa japo kwa mbinde sana)
4. Masters of science in Zoology/ Botany chuo ni UDSM
5. Masters of science with education in Physics/Zoology/ Botany chuo ni UDSM
6. Masters of science in Microbiology au Biotchenology chuo ni UDSM/ SUA
Naomba ushauri na mawazo kwa wajuzi wa haya mambo japo kuna baadhi ya kozi nadhani nikiende kuzisoma mshahara nitakosa ila sitajali sana.
Kama kuna kozi bora zaid na naweza kuisoma bas naomba pia iongezwe kwa wenye ufahamu.
Ahsante, nasubiri mrejesho wako.