Msaada ukubwa banda la kuku wa mayai 500

BABA LEA WATOTO

JF-Expert Member
May 6, 2017
338
722
Habari, naomba kwa wazoefu ni ukubwa kiasi gani kitahitajika kwa ujenzi wa banda la kuku wa mayai wa kisasa 500, pia ningependa kujua vitu muhimu vya kuzingatia wakati wa ujenzi wa banda hilo na mwisho aina nzuri ya kuku wa mayai!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuku 3 hadi 4 wanaweza kukaa eneo la SQM 1, yaani hatua moja urefu na hatua moja upana. Sasa banda la kuku 500 unaweza kufanya hatua 15 urefu na upana 8 linatosha kabisa kuku wako hao.

Je unafuga kuku wa aina gani? tunaweza kukupa ushauri bure!!! Kama ni la matofali basi weka kozi 3 tu, then piga waya hadi kwenye bati, hii inasaidia hewa kupita kwa urahisi kupunguza magonjwa hasa mafua.

Jitahidi usafi bandani pamoja na vyombo vya maji kupunguza magonjwa hasa Mafua, Typhoid na Coccidiosis (Kuhara damu)
 
Mcheki SHAZ KUKUFARM. Anapatikana mbezi beach. Jamaa yuko makini sana kwenye suala la mabanda ya kuku wa aina zote
 
Back
Top Bottom