fokonola bokoyoka
JF-Expert Member
- Feb 13, 2015
- 965
- 640
Habari za mwaka mpya wanajukwaa.
Husika na somo tajwa, mimi ni baba mzazi wa mwanafunzi ambaye alihitimu darasa la saba nikiwa naishi Dar nikifanya biashara ndogondogo kwa bahati nzuri mwanangu amebahatika kuchaguliwa kuendelea na elimu ya sekondari katika moja ya shule ya sekondari iliyopo Dar kwa bahati mbaya baada ya vyuma kukaza ikabidi nirudi kijijini (surrendering) kwa maana ya kwenda kujipanga upya lakini sasa sina ndugu wala jamaa na natamani sana mwanagu (kike) awe karibu ili asije akateseka na kuharibika mjini.
Ninachohitaji kwenu wanajukwaa ni ushauri na utaratibu mzima wa namna ya kumhamishia mkoani kwa maana ya kwamba huku ninapoishi sasa ili mwanangu aweze kufikia malengo yake ya kuwa mwalimu baadae asipobadili mawazo yake ya sasa.
Ushauri wenu kwangu utakuwa msaada mkubwa.
Nawasilisha.