Karibu kwenye ufugaji wa Nyuki, mimi mwenzio sasa Mwaka wa 3.
Kuhusu kuhama kwa nyuki ndani ya mizinga kuna mambo mengi;
1. Utashi wa Asili WA kutaka kuongezeka na kuzaliana, (Kugawanyika Kwa kundi)
2. Uhaba WA chakula,
3.Nafasi ndani ya mzinga kuwa ndogo mno na kuwazuwia nyuki wafanyakazi kushinda kutekeleza majukumu muhimu kama kujenga masega, kuweka Amina ya Asali na kulea watoto.
4. Kuwepo kwa maadui wa nyuki,
5. Matumizi ya dawa za kilimo ambayo yanadhuru nyuki,
6. Hali ya hewa kama joto Kali, baridi Kali, unyevu mwingj na mvua nyingi,
7. Uvunaji usiozingatia kanuni bora, kuvuna masega yote bila kuwaachia nyuki Asali.
Ukiangalia sababu hizi utabaini chanzo cha nyuki wako kuhama, hivyo itakuwa rahisi kusaka ufumbuzi.
Tunaweza kuwasiliana iwapo shida ni kubwa zaidi, nipo Nyuki Farming Mwanza; Call +255622642620