Msaada: Ufahamu kuhusu madini

Yasser5

JF-Expert Member
Mar 15, 2012
207
17
Hi!
Ndugu wana jamvi hili
Naomba nitoeni kwenye kashimo haka, hivi ni madini gani Duniani yenye gharama kubwa.

Ni madini gani yana bei kubwa yanayopatikana Tanzania
Madini aina ya Ruby ni madini ya aina gani na je gharama yake ikoje kwa gram moja?

Msisahu kuniambia wapi kwa Dar maduka ya kununua madini?
 
Tanzania ina madini mengi na ya thamani kama: Ruby, saphire, emarald, diamond, alexandrite, Tanzanite, etc
bei ya madini inategemea na :hardness, size, colour, clearity, na kama yamekatwa na aina ya mkato e.g. brilliant, cushion, oval, table cut etc. Madini yenye bei kubwa kwa Tanzania ni Diamond ikifuatiwa na ruby, emarald, saphire, alexandrite na Tanzanite.
NB. Ruby zipo za aina tatu: red, rose na pink ruby. red ruby ndiyo ya ghali zaidi.
 
Tanzania ina madini mengi na ya dhamani kama: Ruby, saphire, emarald, diamond, alexandrite, Tanzanite, etc
bei ya madini inategemea na :hardness, size, colour, clearity, na kama yamekatwa na aina ya mkato e.g. brilliant, cushion, oval, table cut etc. Madini yenye bei kubwa kwa Tanzania ni Diamond ikifuatiwa na ruby, emarald, saphire, alexandrite na Tanzanite.
NB. Ruby zipo za aina tatu: red, rose na pink ruby. red ruby ndiyo ya ghali zaidi.

Geof unaweza kufunguka kidogo kwa bei kwa ujumla wake kama sio siri Ruby kwa kila gram 1
 
Bei za Ruby : Ruby zote zisizopitisha mwanga (cabochon), ruby nuts, Ruby in Zoisite, Tsavorite etc bei inaanzia dola 10 mpaka dola 500 kwa gram. Ruby yenye kuona, haina chenga, rangi nzuri (pigeon blood ) imekatwa au bado bei inaanzia dola 5,000 mpaka 25,000 kwa jiwe lisiozidi karati mbili. Kwa rough bei inaanzia $ 25000 kwa gram. Bei halisi inategemea na shape ya jiwe, colour, clearity na grade. Wewe una Ruby za aina gani?
 
Tanzanite = Zoisite.
 
Hi!
ndugu wana jamvi hili
Naomba nitoeni kwenye kashimo haka, hivi ni madini gani Duniani yenye gharama kubwa
Ni madini gani yana bei kubwa yanayopatikana Tanzania
Madini aina ya Ruby ni madini ya aina gani na je ghalama yake ikoje kwa gram moja?

Msisahu kuniambia wapi kwa Dar maduka ya kununua madini?
madini yenye thamani kupita yote duniani ni RED GARNETTE.TANZANIA YANAPATIKANA.BEI YA RUBBY SIJUI.MADUKA YA KUNUNUA YAKO KWA WINGI ZAIDI ARUSHA.KAMA UNA RUBBY SERIOUS NI PM
 
gold kumbe iko nyuma tu eheee

Hayo waliyotaja hapo juu ni gemstones(vito), gold ni metal. Huwezi kuanza kulinganisha Gold na Gemstones. Ili kufanya ulinganisho sahihi Gold yapaswa kulinganishwa na metali nyingine mfano shaba na fedha, ambapo Gold ina bei zaidi. Tofauti pia ipo kwenye utafutaji/ uchimbaji wake. Gold ukishafanya exploration una uhakika wa kuipata na inapatikana kwa wingi wakati gemstones ni ya kutafuta, unaweza ukapata au ukakosa.
 
Wakuu,madini ya ruby na saphire yanapatikana Winza-Mpwapwa kwa mhe.Simbachawene;huko wachimbaji wadogo wamezuiwa na wajanja wameingia kwa kishindo! Kazi sasa anayo kamanda Kigaila,kuwatetea walalahoi walioanza kuchimba madini hayo.
 
Bei za Ruby : Ruby zote zisizopitisha mwanga (cabochon), ruby nuts, Ruby in Zoisite, Tsavorite etc bei inaanzia dola 10 mpaka dola 500 kwa gram. Ruby yenye kuona, haina chenga, rangi nzuri (pigeon blood ) imekatwa au bado bei inaanzia dola 5,000 mpaka 25,000 kwa jiwe lisiozidi karati mbili. Kwa rough bei inaanzia $ 25000 kwa gram. Bei halisi inategemea na shape ya jiwe, colour, clearity na grade. Wewe una Ruby za aina gani?
kwa kweri mimi ni mgeni sana katika upandee huu wa madini lakin kwa waloniambia ni red Ruby
 
Piga picha hiyo ruby yako (Jaribu kupiga picha nyingi ili kuonyesha size, colour, clearity, shape etc) halafu mimi kwa kutumia hizo picha nitakupa kisio la bei yake. Bei halisi ya madini yoyote ni lazima mtu ayaone, na kuya-grade kutegemea na vigezo kama nilivyoainisha hapo juu. sababu ni kwamba ruby inafanana sana na spinel-ambayo bei yake iko chini, pia wengine wanauza pink saphire au fake ruby (synthetic ruby) kama natural ruby. Zote hizo zina hardness sawa baliTofauti ya natural ruby na spinel na au synthetic ruby ni density.
 
madini yenye thamani kupita yote duniani ni RED GARNETTE.TANZANIA YANAPATIKANA.BEI YA RUBBY SIJUI.MADUKA YA KUNUNUA YAKO KWA WINGI ZAIDI ARUSHA.KAMA UNA RUBBY SERIOUS NI PM

Sio kweli Mkuu, Red Garnet haina bei kabisa, Green garnet iko mbali sana kwa bei kuishinda hiyo Red garnet, yapo mengi sana kule Ruangwa Lindi yanauzwa kwa kilo
 
madini yenye thamani kupita yote duniani ni RED GARNETTE.TANZANIA YANAPATIKANA.BEI YA RUBBY SIJUI.MADUKA YA KUNUNUA YAKO KWA WINGI ZAIDI ARUSHA.KAMA UNA RUBBY SERIOUS NI PM
Red garnet ipi hiyo mzee? Red garnet ninayoijua mimi kwa jina jingine inaitwa "Almandite" ndugu yake na Pyrope bei yake iko chini sana, na unaweza ukauziwa kilo 1 kwa bei ndogo sana-hata million 4 haifiki. Angalau Rose/Pink garnet in bei lakini bado siyo ya kutisha

Aina ya garnet iliyo ghali sana inaitwa Green Garnet ambayo inapatika landanai na msitu wa tembo kule Arusha.

madini yenye thamani kupita yote duniani ni RED GARNETTE.TANZANIA YANAPATIKANA.BEI YA RUBBY SIJUI.MADUKA YA KUNUNUA YAKO KWA WINGI ZAIDI ARUSHA.KAMA UNA RUBBY SERIOUS NI PM

Mkuu sio kweli Kuwa Red Garnet ndio ina bei kuliko gemstone zote, Green garnet iko juu mara nyingi sana ya hiyo Red garnet,,,,,,,,,,, hizo Red garnet ziko nyingi sana kule Ruangwa-Lindi na zinauzwa kwa kilo tu
 
Back
Top Bottom