Msaada; Tv za kichina nzuri ni zipi?

profesawaaganojipya

JF-Expert Member
Joined
Apr 21, 2015
Posts
1,596
Reaction score
3,439
Naomba kuuliza kwa mafundi na wajuzi, ni TV aina ipi za kichina ni nzuri au zina afadhali, kwa ubora, uimara, picha nzuri nk kushinda nyingine maana nasikia nyingine hazitimii hata zile inches za upana wa kioo.

Kuna MEWE, ALYONS, STAR ONE, STAR X, RISING, TCL, ALITOP, SOLAR MAX NK
 
Mimi ni muuzaji wa TV , ukitaka tv nzuri hakikisha tu unapewa Warranty card imejazwa na ipo verified. Achana na brand , brand zote zinakufa muda wowote, hakuna cha LG wala Samsung, zote ni uchafu
 
1. Singsung
- (Hizi tv Ni roho ya paka miaka nenda miaka rudi), changamoto yake Ni single screen.

2. Tropical
- (skuhz zimeadimika Sana,ila msumari balaa, Bei zake Ni sawa na kina SONY, SAMSUNG N.K). Tunawauziaga sana watu wa serikali na ubalozi.

3. Homebase
- (Ni msumari balaa, Bei yake inakimbizana na kina Hisense, Lg n.k na hawauzii njaa.

4. Goodvision
(Brand ndogo, ila imara na picha quality Sana, baadae itakuja kua brand kubwa sn)

5. Boss
Nazo sio mbaya.

Hizi nyingine ulzotaja Ni za kawaida sana
 
Kuna moja inaitwa Evol sijui nimepata IPO poa sana
 
Mimi ni muuzaji wa TV , ukitaka tv nzuri hakikisha tu unapewa Warranty card imejazwa na ipo verified. Achana na brand , brand zote zinakufa muda wowote, hakuna cha LG wala Samsung, zote ni uchafu
asante kwa ushauri mzuri mkuu..
 
Boss je kati ya tv zifuatazo ipi ina unafuu kwenye ubora ALITOP, SOLARMAX na RISING
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…