msaada tutaniiii!?

sinyaG

Member
Joined
Apr 20, 2013
Posts
26
Reaction score
3
Una dada yako ambaye ni mjamzito baada ya kubakwa na kutokana na hiyo issue kutoa hiyo mimba anataka ila anahofia kuua kiumbe kisicho na hatia tumboni na kuiacha hiyo mimba anataka ila ana hofu huyo mtoto atakuwa anamkumbusha tukio la kubaka kwake sasa utamshauri nini?
Naomba mawazo yenu ndugu zangu.
 
Kama sheria inamruhusu na haitokuwa na madhara ya afya yake kwanini asichukue maamuzi.

Pia kidini..hapa kama ni muislamu inaruhusiwa kama haijafika 3 months sijui wenzetu wakiristo inakuwa vipi?
 
Tunza mimba hiyo wewe sio wa kwanza kubakwa.
Btw kama umebakwa, kwa nini hujafikisha shauri mahakamani?
 
Kama sheria inamruhusu na haitokuwa na madhara ya afya yake kwanini asichukue maamuzi.

Pia kidini..hapa kama ni muislamu inaruhusiwa kama haijafika 3 months sijui wenzetu wakiristo inakuwa vipi?

Usiue...hivyo ndivyo ilivyoandikwa
 
Kuua dhambi jaman! Mbona kuna wengi tu wamefanyiwa kitendo kama hicho na wana amani tu na watoto wao
 
Akubaliane na hali hiyo maana si vyema kuua kiumbe kisicho na hatia. Na kwa kweli si kwamba akidhamilia kuua hicho kiumbe atakiua na yeye kubaki salama. La hasha na yeye aweza kupoteza maisha vilevile. Huo ndo ushauri wangu kwa leo.
 
Huwez jua huyo mtoto atakuwa potential kias gan kwa jamii.kubakwa kunasahaulika,aombe Mungu ampe faraja kupitia huynd mtoto.
 
Two wrong doesn't makes it right,moja kabakwa pili akaabort sio soln ya kuifuta hiyo incidence ilotokea hata nukta

Akubaliane na kilichotokea lkn pia aiset akili yake kutokuwaza hilo tukio na ajifunze kumpenda na kumfurahia mtoto atakaezaliwa sio yy wa kwanza kukutwa na hilo
 
Hiyo mimba asiitoe coz madhara atakayopata akiitoa ni makubwa kuliko akiiacha...! Mbona hayo mambo yakubakwa husahaulika tu... Asifikirie saana ilo tukio akipende hichokiumbe tumboni na Mungu atambariki.
 
Kigezo cha sheria na dini vyote ni unafiki! Madhambi mangapi tunatenda bila kukumbuka dini?!

Afuate moyo wake!

Labda unambie alibakwa akiwa bikira!
 
Kama sheria inamruhusu na haitokuwa na madhara ya afya yake kwanini asichukue maamuzi.

Pia kidini..hapa kama ni muislamu inaruhusiwa kama haijafika 3 months sijui wenzetu wakiristo inakuwa vipi?

sheria ipi unayoizungumzia?na
kuhusu kidini wakristo kuua ni dhambi ndugu yangu
 
Tunza mimba hiyo wewe sio wa kwanza kubakwa.
Btw kama umebakwa, kwa nini hujafikisha shauri mahakamani?

mahakamani kwenda inawezekana ila uoni kuwa ndio atazidi kujitangaza kuwa kabakwa?na watu wengi zaidi watalifahamu hili jambo na jamii itamchukuliaje?
 
Kuua dhambi jaman! Mbona
kuna wengi tu wamefanyiwa kitendo kama hicho na wana amani tu na watoto
wao

Hiyo ni faraja kwangu japo kidogo ila ni kweli hayo usemayo kuwa wapo wenye watoto?walifanyaje hadi wakacope na hii situation?
 
Akubaliane na hali
hiyo maana si vyema kuua kiumbe kisicho na hatia. Na kwa kweli si kwamba
akidhamilia kuua hicho kiumbe atakiua na yeye kubaki salama. La hasha
na yeye aweza kupoteza maisha vilevile. Huo ndo ushauri wangu kwa
leo.

Ahsante kwa ushauri ila huu ushauri usiwe ndio wa mwisho kwa leo cz bado tupo na tutakuwa wegi kwa leo ambao tunahitaji ushauri wako.
 
mahakamani kwenda inawezekana ila uoni kuwa ndio atazidi kujitangaza kuwa kabakwa?na watu wengi zaidi watalifahamu hili jambo na jamii itamchukuliaje?

"Mchelea mwana kulia hulia yeye"...kama angalikuwa ushahidi wa kutosha bado alikuwa na nafasi ya kupeleka mashtaka sehemu husika.
Adui mkubwa namba moja wa haki ni uoga na ndio maana Mh. Gobless Lema hupenda kusema, "Hakuna dhambi kubwa kama Uoga".
 
Kamwe hawezi kusahau hilo tukio hata kama akitoa
Kabakwa na mtu mmja au zaidi?
Namshauri asitoe kwani hakudhamiria na ishakua mimba tayari na ni aibu na fedheha kwa jamii inayomzunguka( kama watu wengi wamelifahamu hilo)
Atafute wanasaikolojia kwa ushauri na aombe Mungu ampe faraja na uvumilivu katka hilo jaribu na ikibidi atoke akaishi mbali na eneo hilo kama inawezekana
Hakuna kinachoshindikana kwa Mungu hata kwake liwe gumu namna gani
Mpe pole sana
 
Ni kukubali matokeo tu, alibakwa then aendelee na maisha na mimba na mtoto wake!
 

Ahsante ila sijui nifnye nn ili akili yangu isiwaze hili jambo?waweza nipa more advice on this pls?duh hapa tu nimechoka kweli kingreza ni witoo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…