Msaada tutani:redanders inahusiana vipi na mshahara wa mtu jamani??? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msaada tutani:redanders inahusiana vipi na mshahara wa mtu jamani???

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by OkSIR, Oct 4, 2009.

 1. O

  OkSIR Senior Member

  #1
  Oct 4, 2009
  Joined: Jun 3, 2009
  Messages: 108
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani naomba niulize kwa wenye uzoefu;hivi mshahara wa mtu unahusianaje na zoezi la redanders??hivi mtu anafanya kazi siku 31 anapitiliz mpaka tar 5 unamwambia pesa yake aipatikani mpaka zoezi zima la kuachishwa kazi likamilike...kwa wale wanaojua sheria jamani embu tuwasaidie ndugu zetu hawa wa ATCL ; kampuni imeanza zoezi la redanders;baya zaidi wake zetu wamekataliwa kupewa mshahara mpaka zoezi la redanders liishe...je hii ni haki??kwa nini watu waumizwe kwa matatizo yasiyowahusu??
  je wafanyakazi ndio waliolazimisha kufikia hapo ilipo
  iweje watu wachache waumizwe huku wengine wakineemeka??

  WANA jf TUNAOMBA MSAADA WA KISHERIA
   
 2. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #2
  Oct 4, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,485
  Likes Received: 5,721
  Trophy Points: 280
  Hao watu hata awasaidiki ndugu yangu;kwanza tatizo kubwa linaanzia kwa wafanyakazi..wote waoga hakuna hata mmoja anaweza kuamua tunataka hiki..tatizo kubwa nahisi wengi hawajui sheria na haki zao..hakuna kitu kizuri kama kujua haki yako...kama wangalijua hili tarehe 30 hakuna kufanya kazi;tena wameambiwa kabisa late retrechment no salary...sasa kama wanaendelea na kazi mpaka sasa wanaitaji msaada gani???
   
 3. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #3
  Oct 4, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,485
  Likes Received: 5,721
  Trophy Points: 280
  kama mkeo kachelewa kukuletea salary slip mwambie asiende kazini kabisa;hilo ndio soln
  kuna njia nyingi tu....
   
 4. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #4
  Oct 4, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,485
  Likes Received: 5,721
  Trophy Points: 280
  Ndoa ndoano
   
 5. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #5
  Oct 4, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,485
  Likes Received: 5,721
  Trophy Points: 280
  Duuuuh kazi kweli kweli;;;;
  hivi ndugu yangu mattaka nae amebaki!?????kila mbuzi na urefu wa kamba yake
   
 6. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #6
  Oct 4, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,485
  Likes Received: 5,721
  Trophy Points: 280
  Wachezaji wote wa timu ya kwanza ya Portsmouth inayoshiriki ligi kuu ya Uingereza jana hawakulipwa mishahara yao kama kawaida, jambo ambalo likezua utata mkubwa.

  Meneja mkuu wa timu hio Paul Hart asubuhi hii amekalishwa kikao na wachezaji wakidai majibu ya kwanini mishiko yao haijaingizwa kwenye akaunti zao jana.

  Timu hio ya Portsmouth yenye makazi yake katika mji wenye bandari ya Portsmouth kusini mwa Uingereza kwa sasa inamilikiwa na Sulaiman Al FahiM baada ya kufanikiwa kuinunua kutoka kwa mwekezaji mwingine Alexandre Gaydamak kwa kiasi cha paundi milioni 60.

  Sulaiman Al FahiM mwenye asili ya uarabuni aliinunua timu hiyo mwishoni mwa mwezi June mwaka huu huku akiahidi kuwekeza kiasi cha paundi milioni 50 na kuinyanyua kimapato timu hio na kuhakikisha kwamba timu hio inakwa na uwanja mpya na mkubwa kuaidia mapato kutoka ule wa Fratton Park.

  Lakini hadi sasa bwana Sulaiman Al FahiM ameshindwa kupata paundi milioni 2 ili kuweza kulipa mishahara hio na wachezaji hasa wale wageni wamechukizwa sana na mtindo huu.

  Haya hivyo taarifa za ndani ya timu hiyo zinasema kwamba wachezaji watalipwa ndani ya masaa 48 yajayo.

  Timu hiyo inachezewa na kipa wa Uingereza David James ambae ni mkongwe kwa sasa pia na nahodha wa timu ya taifa ya South Africa Aaron Makoena ambae ndie mkoba, mshambuliaji Nwanko Kanu ambae pia anazungumzia kuhamia Australia kucheza soka la kulipwa, Younes Kaboul ambae alitemwa na Tottenham, mchezaji mpya Tommy Smith ambae ametokea Watford na Aruna Dindane ambae ni kiungo wa timu ya taifa ya Ivory Coast.

  Wengine ni pamoja na Muisraeli Tal Ben Haim na Kevin-Prince Boateng ambae ni Mjerumani mwenye asili ya Ghana na mwenye uraia wa nchi mbili ambae ametokea timu ya Hertha Berlin ya Ujerumani.

  Timu ya Portsmouth katika msimu wa usajili mwaka huu ilikuwa ni timu iliokuwa "busy" sana kuuza wachezaji wake wakiwemo washabuliaji wawili Peter Crouch na Jermain Defoe ambao pamoja na mchezaji wa kiungo Nico Kranjcar walijiunga na timu ya Tottenham Hotspur ya Kaskazini Mashariki mwa London ambayo kocha wake Harry Redknapp aliwahi kuifundisha Portsmouth.

  Mchezaji mwingine ni Glen Johnson ambae ni beki wa kulia wa timu ya taia ya Uingereza ambae alinunuliwa na timu ya Liverpool kwa kiasi kisichopungua milioni 25.

  Mshahara kwa ujumla kwa wachezaji ni si chini ya paundi milioni 30 na mpaka sasa kunahitajika kiasi cha paundi milioni 75 ili kukidhi mahitaji yote ya mishahara na biashara zingine.
  __________________
   
Loading...