Msaada Tutani: Mafunzo ya ufundi kwa walemavu wa macho!

jogoo dume

Member
May 12, 2014
70
77
Natumaini msomaji haujambo,naleta kwenu ombi la kuelimishwa/kufahamishwa.

Nna mdogo wangu wa kike aliyemaliza kidato cha nne mwaka jana ambaye ana ulemavu wa macho(Blind). Matokeo yake hayampi nafasi ya kuendelea na A level.

Nimejaribu kutafuta mtandaoni chuo ambacho anaweza kupata mafunzo ya ufundi hapa tanzania bila mafanikio.

Hivyo naomba yeyote mwenye uelewa/kufahamu wapi kuna chuo kinachotoa mafunzo ya ufundi kwa walemavu wa macho hapa Tanzania anijulishe.

Natanguliza shukrani kwa kuchukua muda wako na kusoma.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jaribu kwenda kwenye taasisi yao moja iko kinondoni, shuka manyanya nenda kama unaelekea shule ya kinondoni au Kota za kinondoni.... Hapo ukifika utapata msaada na taarifa zote

Ova

Sent using Jamii Forums mobile app
Kweli mkuu karbu na maeneo ya shule ya kambangwa pale huwaga nawaona walemavu wengi wa macho kumbe kuna taasisi maeneo yale

yess BiShoo haswaaAaa
 
Back
Top Bottom