Msaada tutani flight kutoka KIA (Kilimanjaro international airport) mpaka Frankfurt Germany sijui kitu

sidsel Nelsen

New Member
Sep 19, 2018
3
3
Habari zenu wakuu

Naombeni msaada wa maelekezo kuhusu kupanda ndege maana Nina mawazo mno

Kiufupi sijawahi panda ndege tokea nizaliwe sijui chochote! Nasafiri mwenyewe kutoka Kilimanjaro aiport mpaka dar alafu dar mpaka Amsterdam kutoka hapo mpaka Frankfurt hapo nitakutana na mwenyeji wangu
Hayo Ndo maelezo ya ticket yangu

Najiuliza hizi layover nitafanya nini? Nina masaa 14 Amsterdam na ninaskia ni uwanja mkubwa unapanda usafiri kabisaa kutoka sehemu moja kwenda nyingine! (naogopa ntapotea Mimi) au kuachwa na ndege

Sijui hata kucheck in hata chochote sintapotea huko katikati au kupoteza mabegi? Sijui hata Hali za hewa huko niendako nsije kufa kwa baridi kwenye hizo layover?

Nimejaribu kupitia baadhi ya nyuzi sielewi naomba mnieleweshe vizuri maana kadri siku zinavosogea nazidi kupagawa natamani kuahirisha! Nasafiri ndani December mwanzoni

Naombeni maelekezo pia Kama Kuna vitu vya muhimu vya kununua ninunue?
Hongera pia kwa wale walizoea kupanda ndege tokea utotoni na wazazi wao!

NB: ID ya zamani Ipo lakini muhimu ni kusaidiana Sio kuchambana ..mrejesho utakuja pia

Asanteni mmbarikiwe sana
 
Kila kitu kina siku yake ya kwanza kukifanya kwny maisha,tafuta huu uzi humu jf unaitwa

"Viroja siku ya kwanza kupanda ndege"

Utajifunza mengi mtoa mada,all the best mkuu kwny hio safari.
 
Layover masaa 14 nadhani watakupa hotel ya kupumzika. Ila mbona ni muda mrefu sana ilhali ndege kwenda sehemu za ulaya zipo muda wowote tu.
 
Habari zenu wakuu

Naombeni msaada wa maelekezo kuhusu kupanda ndege maana Nina mawazo mno

Kiufupi sijawahi panda ndege tokea nizaliwe sijui chochote! Nasafiri mwenyewe kutoka Kilimanjaro aiport mpaka dar alafu dar mpaka Amsterdam kutoka hapo mpaka Frankfurt hapo nitakutana na mwenyeji wangu
Hayo Ndo maelezo ya ticket yangu

Najiuliza hizi layover nitafanya nini? Nina masaa 14 Amsterdam na ninaskia ni uwanja mkubwa unapanda usafiri kabisaa kutoka sehemu moja kwenda nyingine! (naogopa ntapotea Mimi) au kuachwa na ndege

Sijui hata kucheck in hata chochote sintapotea huko katikati au kupoteza mabegi? Sijui hata Hali za hewa huko niendako nsije kufa kwa baridi kwenye hizo layover?

Nimejaribu kupitia baadhi ya nyuzi sielewi naomba mnieleweshe vizuri maana kadri siku zinavosogea nazidi kupagawa natamani kuahirisha! Nasafiri ndani December mwanzoni

Naombeni maelekezo pia Kama Kuna vitu vya muhimu vya kununua ninunue?
Hongera pia kwa wale walizoea kupanda ndege tokea utotoni na wazazi wao!

NB: ID ya zamani Ipo lakini muhimu ni kusaidiana Sio kuchambana ..mrejesho utakuja pia

Asanteni mmbarikiwe sana
poleni sana utazoea tu, subiri wajuzi waje!
 
Mkuu issue kumbwa ni kua unaweza kuongea

Humu ktk usafir hutakua peke yako utakutana na wa tz wenzako ila hata kama sio mtz

Ukishakua unajua ku dodosa english basi utaenda popote dunian vzur tu ukishakua na hela na mawasiliano

Ktk airpots kuna wi-fe so hakikisha smu yako inakua on in case for emergence
 
Tiketi umekata mwenyewe au umekatiwa na mwenyeji wako? Je na malazi ya hotelini kwa huo muda wa masaa 14 ni sehemu ya nauli (tiketi) uliyonunua? Amsterdam na Frankfort sio mbali, na ndege za kumwaga kila baada ya kipindi kifupi zinaelekea huko, sielewi kwa nini unakaa masaa yote hayo hapo Amsterdam?
Kupotea si rahisi, kwenye tiketi kuna namba ya ndege na mji unaokwenda, hivyo ukiwa Amsterdam, kuna screen kubwa ukutani kwenye corridors, angalia ya departures, angalia mji unaoelekea, imepangwa kwa alfaberi, kama namba ya ndege inaendana na ile kwenye tiketi yako, basi angalia wanapakia geti gani na saa ngapi. Kulingana na hapo ulipo, unafuata au kuuliza wafanyakazi walio kwenye sare zao za Klm au Schipol airport wapi lilipo hilo geti, au unafuata maelekezo yaliyobandikwa kwenye corridors. Ila kama una masaa 14 ya kuunganisha ndege, utakapofika hutaona maelezo ya ndege yako ya siku inayofuata katika hizo screens, hivyo itakubidi uwaulize wahudumu waliokaa katika madawati ya kutoa huduma. Maelezo katika screen ni ya ndege zinazoondoka au kuwasili masaa machache kabla muda husika.
 
Ukifika airport kuna matangazo ya flight husika mkuu, Mimi nilienda hapo mwanza tuu lakini nilifuata niliowakuta pale airport very easy
 
Tiketi umekata mwenyewe au umekatiwa na mwenyeji wako? Je na malazi ya hotelini kwa huo muda wa masaa 14 ni sehemu ya nauli (tiketi) uliyonunua? Amsterdam na Frankfort sio mbali, na ndege za kumwaga kila baada ya kipindi kifupi zinaelekea huko, sielewi kwa nini unakaa masaa yote hayo hapo Amsterdam?
Kupotea si rahisi, kwenye tiketi kuna namba ya ndege na mji unaokwenda, hivyo ukiwa Amsterdam, kuna screen kubwa ukutani kwenye corridors, angalia ya departures, angalia mji unaoelekea, imepangwa kwa alfaberi, kama nsmbavya ndege inaendana na ile kwenye tiketi yako, basi angalia wanapakia geti gani na saa ngapi. Kulingana na hapo ulipo, unafuata au kuuliza wafanyakazi walio kwenye sare zao za Klm au Schipol airport wapi lilipo hilo geti, au unafuata maelekezo yaliyobandikwa kwenye corridors. Ila kama una masaa 14 ya kulinganisha ndege, utakapofika hutaona maelezo ya ndege yako ya siku inayofuata katika hizo screens, hivyo itakubidi uwaulize wahudumu wanataka katika madawati ya kutoa huduma. Maelezo katika screen ni ya ndege zinazoondoka au kuwasili masaa machache kabla muda husika.
Huyu mdau amekusaidia sana usitafute mwingine. Lakini cha ajabu kwa nini masaa 14? Hebu fuatilia hilo Bwana.
Safari njema
 
  • Thanks
Reactions: Auz
Habari zenu wakuu

Naombeni msaada wa maelekezo kuhusu kupanda ndege maana Nina mawazo mno

Kiufupi sijawahi panda ndege tokea nizaliwe sijui chochote! Nasafiri mwenyewe kutoka Kilimanjaro aiport mpaka dar alafu dar mpaka Amsterdam kutoka hapo mpaka Frankfurt hapo nitakutana na mwenyeji wangu
Hayo Ndo maelezo ya ticket yangu

Najiuliza hizi layover nitafanya nini? Nina masaa 14 Amsterdam na ninaskia ni uwanja mkubwa unapanda usafiri kabisaa kutoka sehemu moja kwenda nyingine! (naogopa ntapotea Mimi) au kuachwa na ndege

Sijui hata kucheck in hata chochote sintapotea huko katikati au kupoteza mabegi? Sijui hata Hali za hewa huko niendako nsije kufa kwa baridi kwenye hizo layover?

Nimejaribu kupitia baadhi ya nyuzi sielewi naomba mnieleweshe vizuri maana kadri siku zinavosogea nazidi kupagawa natamani kuahirisha! Nasafiri ndani December mwanzoni

Naombeni maelekezo pia Kama Kuna vitu vya muhimu vya kununua ninunue?
Hongera pia kwa wale walizoea kupanda ndege tokea utotoni na wazazi wao!

NB: ID ya zamani Ipo lakini muhimu ni kusaidiana Sio kuchambana ..mrejesho utakuja pia

Asanteni mmbarikiwe sana

Unaondoka na ndege gani?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom