hivi chief specification za hii simu kama c9. ukilinganisha na simu za kampuni nyingne kama iphone, sony, sumsung au lg bei yake ni shingapi.
mkuu matatizo ya simu za mediatek moja wapo ni kwamba hazina balance ya specs,
mfano cpu ya hii c9 sio mbaya inafanana na simu kama j7 au midrange za huawei kama honor 5x hivi.
ukija gpu ndio mehhh!! gpu yake ni mali 400mp2, kwa ulinganishi galaxy s3 gpu yake ni mali 400mp4, hizo mp zinamaanisha core za graphics s3 gpu yake ina core 4 wakati c9 ni core 2 hivyo gpu ya c9 ni dhaifu zaidi ya s3 simu ya mwaka 2012. halafu kibaya zaidi wakaeka na kioo cha full hd kwenye gpu hio.
hivyo huwezi fanya direct comparison na simu za kampuni kubwa
japo hii simu imezidiwa kila idara na midrange za kampuni kubwa kama huawei na samsung, yenyewe inauzwa bei ghali zaidi. ila sababu watu wamekariri tecno ni bei rahisi wanainunua hali ya kuwa hawajui.
hizi ni baadhi ya simu za kampuni kubwa zinazocompete na c9
-galaxy j5 na j7 (version za 2016 ni nzur zaidi)
-huawei honor 5x
-huawei g8
-motorola g4
etc
pia zipo simu za makampuni makubwa ya china (ukitoa huawei) kama xiaomi redmi note 3 ambazo zina specs kali kushinda tecno yoyote iliyopata kutengenezwa (nzuri kuliko phantom z5) kwa bei around dola 150. hizi zipo kenya bei kama laki 4 ya tz