Za mchana wakuu na wanajamvi kwa ujumla. Nina shida na nnaimani mtanipa ushirikiano katika kutatua shida hii. Ni hivi mwaka huu nimeomba vyuo kwa Mara ya pili na masharti yoote ya kuandika barua kwenda TCU inayoelezea sababu zilizo ni nyima kwenda chuo kwa mda huo (2012).Sikuweza kupata barua kutoka chuo nilichopangiwa hapo awali kwani waliniambia wenye shida kama yangu ni wengi hivyo kuna utaratibu wakuchukua majina na kuyaandikia barua ya pamoja (kutoka chuoni kwenda TCU).Juzi jumatatu nilienda TCU na wakani dhibitishia kuwa walishapata majina kutoka chuo nilicho pangiwa awali hvyo wakanihakikishia ndani ya week hii watatangaza butch 4 Jana niliangalia majina yaliyotoka yaaani butch4 cha kusikitisha sikuona jina langu. Mda unazidi kwenda na waombaji wanazidi kuongezaka je nifanyeje kwani kama ni kutinga kwenye ofisi za TCU nimechoka.Nifanye je ili nipate admission kiukweli najisikia kama nachanganyikiwa hivi