Naona kitu ile inaitwa PILOTING (Majaribio) ni tatizo kwetu (TCU, NACTE, NECTA, Vyuo) yaani mtu anakuja na mfumo mpya bila kuufanyia majaribio ya kutosha, na hasa shinikizo linapotoka kwa wakubwa inabidi bora liende. Kumbukeni JPM ndiye alie agiza vijana wachague chuo na course moja kwa moja ili wapate wanachokipenda na sio "kupangiwa" na TCU - na TCU kwao ilibakia utekelezaji, MULTIPLE SELECTION zikatesa sana vijana kwenye ku-konfem, mikopo na course (wapo wengi tu mambo yalipokaa vibaya walijipachika tu ili wasikose vyuo. Mwaka huu tena MULTIPLE SELECTION mwiba. Mwaka huu ni MULTIPLE SELECTION na mdogo wake CONFIRMATION CODES (kuzipata na kuuzingiiza imekuwa shida).
Tunawasema admission desks lakini nina hakika na wao cha moto wanakiona, kwani kila chuo kinajitahidi kupata wanafunzi issue ni je wana watu wa kutosha na technolojia inayojitosheleza. Sidhani.