Msaada tatizo la low voltage

Realbest

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2013
Posts
812
Reaction score
303
Habari wakuu?

Hapa kwangu nilipohamia pana tatizo la nyumba nyingi zina low voltage.

Ni kifaa gani kinaweza kufaa kubalance umeme angalau niwe natumia Tv, Radio na matumizi madogo ya hapa nyumbani? Nimenunua volt Guard lakini inajizimazima hovyo ikifika muda ya jioni.

Mbali na stabilizer, hiki kifaa hapa chini kina kazi gani? Je kinaweza kuwa mbadala wa tatizo langu?

Nawasilisha.

 
Kama tatizo la under voltage mnalipata wengi looks hilo tatizo huwezi kulisolve wewe, otherwise lingekua kwako.

Hapo shida ni kwamba inaonekana ninyi wote mumekua connected katika phase moja ya tanesco say R, Y or B sasa imekua loaded mpaka voltage ikawa below 230V,

Solutions:
1. Tanesco wanakuja kubalance kwa kuwahamisha wateja baadhi kwenye phase nyingine, hapo itapanda mpaka 230V
2. Kwa kubadirisha tap changer ya transformer ili kustabilize 230V


Otherwise kama kuna kingine unaweza kusema tukusaidie

Regards,
Engineer.
 
Nakushukuru Mkuu na je Kazi ya kifaa hiki ni ipi?
 
Nakushukuru Mkuu na je Kazi ya kifaa hiki ni ipi? View attachment 1266190
Kazi yake ni kumaintain voltage ambayo uta SET hapo. Yaani ukiset 230V inamaintain hiihii au any voltage set (SP=Set Point) ili kukilinda kifaa kinacho tumia 230V kisiwe damaged na overvoltage, undervoltage na hata overcurrent(optional). Kitaalamu tunaita PID voltage Controller, Ni kama AVR au stabilizer wengine huita regulator wakati sio. PID controller hii ni digital one means inatumia more digital electronics components na algorithm/software kuliko analogy components kama conventional zilivyo. Business name naona wameita Adjustable Voltage Protector means protection against any swing voltage over the equipment being used. Hii inaweza kufanya hata kazi ya LUKU meter kwa kudisplay kWh (units) za kifaa TV, etc zilizotumika but inadepend za umechukua type gani, read the datasheet of it before buying.



As long as law of conservation of energy is concerned!.

Chukulia electricity working ni analogous na maji

Uki SET maji lita 20 yakiingia pipa basi hichi kifaa Kita maintain lita 20 ndo zibaki na sio pipa hapa nikama overvoltage imeshushwa mpaka 230V ambayo already SET.

UkiSET maji lita 20 na yakaingia lita 5 basi hichi kifaa hakiwezi kuzalisha maji lita 15 extra ili yawe maintained yakiwa lita 20, tatizo linakua maji yalipotoka nimachache kiasi hayawezi kua computed mpaka yabaki lita 20, hapa nisawa na supply ya tanesco ni under 200V halafu unataka imaintain 230V, rejea law of conservation of energy. So kama Voltage hata kifaa kinashindwa ku maintain basi tatizo linaeza kuwa supply voltage pia.


Karibu,

Engineer.
 
Injinia hapo umemaliza kila kitu! Ahsante Sana maswali yangu yamejibiwa nandyo maana humu namuamini vilivyo
 
Mkuu kwa changamoto yako option ulizonazo ni either ureport tanesco waje wafanye Adjustment kwenye tap changer au kama imepita three phase kawaombe waje wakuhamishe Phase. Tatizo hilo ni common sana maeneo mengi haswa nyakati za jioni na huwakuta zaidi wateja walio ktk phase ya tatu (BLUE) Huletwa na Inbalance inayofanywa na tanesco kwa urahisi wa kuconnect hio phase ya tatu.
 
Ahsante mkuu kwa nitaufanyia kazi ushauri wenu
 
Yaaaani umesomeka sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…