Anyway, japo mimi si mtabiri nyota lakini kuna kitu nitasema hapo hasa kwa kuzingatia mambo machache tu. Mosi, Mungu huwa anasema na watu kwa namna mbalimbali hasa kwa ndoto ili kukuonya mwenendo wako au kukubariki kulingana na matendo yako. Pili ndoto zingine mtu anaweza ota kwa sababu tu ya kumbukumbu nyingi zilizohifadhiwa kwenye hard disk yake yaani ubongo. Tatu, shetani anatumia mwanya huo kukuotesha mindoto fulani ili aweze kujiunganisha ama kufanya mikataba laghai na mhusika kwa manufaa yake mwenyewe. Ok, nisikuchoshe. nitaanza na ndoto ya pili ni kuwa makini sana na hali ya kiuchumi yako yaani tumia pesa vizuri; usifuje hicho kidogo unachopata. Kwa maana nyingine waweza poteza bahati fulani hivi karibuni au huko mbeleni. Kwanini nasema hivi, ni kwamba ungeliota unapewa pesa hiyo ingemaanisha utapata baraka fulani hivi karibuni. Naaa, ile kuhusu ndoto ya mwanzo haina maana nzuri sana kwako kwa mtizamo wangu au mawazo yangu (Wana JF, don't judge me on that). Kifupi embu kuwa makini au omba mara kwa mara kwa Mungu kwa imani yoyote ili akuepushe na ajali, mikosi. Halafu pia kuna mtu fulani ukakutana naye sijui kavaa vitu gani anyway sijui ni mtego huo ndio wakala wa shetani alikuwa anataka kuingia mikataba mibofu mibofu na wewe. So suit yourself.