Dupe
JF-Expert Member
- Jan 21, 2013
- 1,668
- 811
Ilikuwa ni usiku wa jana kuamkia leo nilipojikuta naingia kwenye ndoto ambayo mpaka sasa sijapata kujua ikomaanisha nini.
Ndoto Yenyewe:
Tulikuwa watu wawili yaani nimimi na mdogo wangu, mdogo wangu aliniomba nimsindikize mahala fulani ambaki mpaka sasa sipajua palikuwa wapi…!!
Tulifika kwenye hiyo nyumba tukaingia ndani ile nyumba ilikuwa haijaisha kwa kujengwa, yaani mithili ya mtu akiejenga alikuwa kaishindwa so watu wakapangishwa, mdogo wangu alikuwa mbele yangu maana ye ndio alijua wapi tunaenda.
Katika hiyo nyumba ilikuwa ina milango kama nane, yote ilikuwa inaangaliana. Tukapita katikati hadi kwenye mlango wa mwisho wa kushoto wa mkono wetu. Mule kwenye kile chumba hakukuwa na mtu yeyote na mdogo wangu aliingia mpaka ndani na akatoka haraka, mie nikiishia mlangoni pasi kuona ni nini alikiona mule ndani au ndani kulikuwa na nini! Niliona kitanda tu, ambacho kilikuwa na shuka jeupe.
Nilipoona mdogo wangu katoka nami niligeuza paleplale. Wakati tunatoka kabla hatujaimaliza ile nyumba kutoka, yule mwenye chumba ambacho tuliingia akawa anaingia ndani na yeye. Yule mdogo wangu alipomuona alikuwa anacheka na akakimbia huku akiniacha nyuma nikipigwa na butwaa…!!
Yule mama alisimama akaniangalia akaingia chumban kwake na akarudi tena, aliporudi alinikuta mimi nikitoka pale, akanifuata akasimama mbele yangu huku akinitazama kwa hasira…!!
Akachukua mikaa mitatu akanipiga nayo kifuani halafu akanisonya na kuniambia "Ole wenu mukasimulie…!!".
Hapa ndipo nilipochanganyikiwa kabisa mpaka sasa na sijajua nyumba ambayo tuliingia iko wapi na yule mama alienichimba mkwala simjui.
Naomba msaada wa tafsiri wa ndoto hii waungwana..
cc: Mshana Jr
cc: MziziMkavu