Msaada: Tafsiri ya ndoto hii

Msaada: Tafsiri ya ndoto hii

MWAMUNU

JF-Expert Member
Joined
Dec 17, 2011
Posts
866
Reaction score
526
Heshima kwenu wakubwa zangu, na madogo hamjambo.

Niende moja kwa moja kwenye hoja.

Asubuhi hii saa 12 nimeota ndoto ambayo inaninyima raha sana, .

Katika ndoto hiyo nimeota nimesingiziwa nimeiba box 9 za karatasi nyeupe yaani rim paper na kufungwa miaka miwili jela

Nikiwa jela napata taarifa kwamba jamaa yangu kipenzi (jina namhifadhi)amefariki dunia, nasikitika na kumlilia sana.

Baada ya kumaliza kifungo siku hiyo hiyo naingia mtaani huku ndugu na jamaa wakiendelea kunipa pole, mara jamaa yangu niliyeambiwa amefariki nae anatokea na kunipa pole, namuuliza we si nimeambiwa umekufa ananijibu achana nao wanafiki hao.

Namuuliza umejuaje nimetoka ananijibu fulani(Jina namhifadhi) kakusanya watu anawasimulia watu kwamba uliiba box 9 za karatasi na kwamba walihakikisha hutoki hata kama una uwezo wa kuzilipa.

Ikumbukwe huyo jamaa anayeninenea mabaya huku kwenye maisha ya kawaida ni Mzee wa kanisa na ndie aliesimamia ndoa yangu, japo ilishavunjika, Mwisho wa ndoto yangu.

Wakuu kama kuna wajuzi wa kufafanua ndoto naomba msaada hii ndoto ina maana gani?

Nimeota asubuhi hii na nakumbuka kila kitu yaaani kama movie vile.

Natanguliza shukrani, kama huna la kuchangia pita kimya kimya.
 
Hii itakuwa na maana Sana .

Karatasi nyeupe: huenda Ni usafi au ukamilifu wa jambo

Kifungo ; kurekebisha Tabia au adhabu .

Kusingiziwa kifo ; wivu kutopenda maendeleo ya mwingine.

Huo Ni mtazamo wangu tu , sasa kiunganishi hizo dots ndo ishu. Anyway wataalamu watafika hapa
 
Kwanza ningetamani kujua Wewe unafanya kazi gani? Lakini pia umegusa kanisa je huko una cheo gani Ni mzee wa kanisa muimbaji,kiongozi wa vijana n k.

Kitendo Cha kuota ndoto umesingiziwa kuiba ni kwamba jamii inayokuzunguka Kuna Watu wanaokuonea wivu kwa sababu wanakuona unatishia masilahi yao. Lakini mpaka unahukumiwa kifungo Cha miaka miwili,inaonyesha unaweza upate safari either ya masomo au uhamisho kikazi utakaokuondea hapo ulipo kwa miaka miwili.

Kama una mchumba au mke huyo rafiki yako wa karibu atakusaliti atatembea na huyo mke wako au mchumba wako. Omba Sana damu ya Yesu ikufunike ili hao wanao kuwazia mabaya washindwe kwa jina la Yesu
 
Kwa Waandishi wa Bongo movie... Hii ni bonge moja ya story nzuri sana. Mje muombe ithibati, Hii story ni nzuri sana.
 
kitu cha kusingiziwa, ndo unafungwa na jela bila ushahidi khaaaa
hiyo ndoto ya asubuhi au mchana ??
 
kitu cha kusingiziwa, ndo unafungwa na jela bila ushahidi khaaaa
hiyo ndoto ya asubuhi au mchana ??
Kaka si unajua mambo ya ndoto? Mda mmoja utakuta mara upo singida , mara upo Mwanza, mara upo ulaya japo hukujui,kwenye hii ndoto nlikua kabisa naona nimeonewa!!
 
kuwa makin na marafiki na watu wanao kuzunguka..hamna uwakika kwamba ndoto inaweza tokea kwel ,bila shaka utakuwa unafanya kazi sector ya elimu adi umeota makaratasi(rim paper) kwann usingeota unarusha ndege?
 
Usirelax, ndoto ni halisi na maisha ya kawaida mara nyingi huanzia rohoni. Kwa uelewa wangu mdogo ni kuwa umepewa taarifa kuwa kuna jambo utasingiziwa, yaweza isiwe kuiba ream lakini chochote na atakayekusingizia ni mtu wa karibu na unayemuamini.
Sasa tuje kwenye point: je nini lengo hasa la taarifa?
Lengo la taarifa ni kukuhabarisha, kukupa fursa ya kukataa unachoambiwa au kukubali. Ndio maana kwenye mambo ya kiroho tunaambiwa unaweza kukataa au kukubali ndoto unayoota.\
Ushauri wangu, ingia maombi ya kumaanisha/kufunga kataa hiyo scandal iliyoandaliwa kukuabisha au kukutesa. Mungu ataiondoa
 
Asante mkuu ntalifanyia kazi
 
Aisee, Mimi sitaki kuota tena, kama shabiki wa Simba siku mbili kabla ya mechi niliota tumefungwa goli moja na kwenye ndoto niliona Simba akiangaika sana, hadi naamka simba alikuwa akiangaika, japo ndoto iliisha lakini mwisho wa mechi sikufikia.
 
Kaka si unajua mambo ya ndoto? Mda mmoja utakuta mara upo singida , mara upo Mwanza, mara upo ulaya japo hukujui,kwenye hii ndoto nlikua kabisa naona nimeonewa!!
Kiroho ukilala roho huwa inasafiri inaacha mwili na kwenda kutembea sehemu ulizoziota,roho ikikutana na jeruhi lolote huko ilipo upelekea kifo cha usingizini3.
 
Kwanza ningetamani kujua Wewe unafanya kazi gani? Lakini pia umegusa kanisa je huko una cheo gani Ni mzee wa kanisa muimbaji,kiongozi wa vijana n k.

Kitendo Cha kuota ndoto umesingiziwa kuiba ni kwamba jamii inayokuzunguka Kuna Watu wanaokuonea wivu kwa sababu wanakuona unatishia masilahi yao. Lakini mpaka unahukumiwa kifungo Cha miaka miwili,inaonyesha unaweza upate safari either ya masomo au uhamisho kikazi utakaokuondea hapo ulipo kwa miaka miwili.

Kama una mchumba au mke huyo rafiki yako wa karibu atakusaliti atatembea na huyo mke wako au mchumba wako. Omba Sana damu ya Yesu ikufunike ili hao wanao kuwazia mabaya washindwe kwa jina la Yesu
Heshima kwako mkuu ... naomba nami nisaidie hii ndoto ... jana usiku nimeota tunasafiri usafiri wa basi (eacher) kuna sehem tulifika ikatubidi mimi na baadhi ya abiria tushuke tukaingojee gari kwa mbele sasa wakati tuna tembea ikaonekana kama tupo sehem hatarishi sana kuna vibaka wengi wanaojidunga sindano za madawa ya kulevya na moja ya watu tulio shuka nao pia ni mtumiaji kwahiyo tuka fika sehemu tuka mkuta simba huyo simba yupo kama amekatwa upande yani sehemu ya mwili wa simba upo chini lakini sehemu ya mkia na kipande kidogo ndo ina onekana ina cheza ... basi yule ndugu(simfahamu) ikawa nikama anawapelekea wale vibaka wezake mzigo flani akaomba nimsindikize kule japo nlikiwa na hofu sana nikamsindikiza kufika kule nika mwambia mimi siingi humo yeye akaingia ... alipo ingia tu aka tekwa na wale vibaka nikarudi haraka kwa wale abiria wenzangu kuwapa tarifa basi tukawa tuna sikitika pale hadi nikashtuka
NB: nimekuwa nikiota ndoto za safari mara kwa mara ,ndoto za shule ya msingi mara kwa mara , ndoto za kukamatwa au kuwa na polisi mara kwa mara, ndoto za kuwa kijijini na vuka mito mara kwa mara , ndoto za kuwa karibu na rais hasa marehem MKAPA mara kwa mara, ndoto nikiwa na daimondplatnums mara kwa mara, ndoto naokota dhahabu ,mara kwa mara, ndoto nakula matunda mara kwa mara ....@Mshana jr
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom