JT wa Dommy
Member
- Sep 15, 2016
- 29
- 38
Habari wapendwa. Nimekuwa nikiota hizi ndoto za nyoka mfululizo nashindwa kuelewa kwanini.
Juzi niliota niko kwenye nyumba imezingirwa na nyoka wa aina tofauti wengine hata sijawahi kuwaona wa ajabuajabu wapo kwenye kila chumba isipokuwa chumba tulichokuwepo sisi (nilikuwa na watu wengine kama 5) wakati tunajiuliza tufanyeje nikaamka.
Leo nimeota wakati nazunguuka nyuma ya nyumba yetu kukagua kagua (nyumba yenyewe haifanani na ya kwetu kiuhalisia) nimedumbukia kwenye kisima kidogo kilichojaa nyoka wadogowadogo wengi sana ila kwa bahati nzuri nikajivuta juu nikatoka. Nilishtuka nikaamka ila baada ya muda kidogo nikalala tena nikaota kuna linyoka likubwa sana halafu mweusi sana kuna watu wanapambana nalo, mimi lakini nimesimama kwa mbali naangalia, kwenye hao watu wanaohangaika kumdhibiti huyo nyoka kuna msichana ambaye yupo na mbwa wake bahati mbaya yule nyoka akamng'ata mbwa. watu wa pembeni yangu wakawa wanasema huyo mbwa hawezi pona maana yule nyoka ni black mamba akikuuma unakufa hapohapo. Na ni kweli sekunde chache tu mbwa akafa. Na mimi nikaamka
Sasa jamani sielewi hizi ndoto zinamaanisha nini kwa kweli ningekuwa nimeangalia kipindi cha wanyama au movie ya kutisha au chochote kuhusu nyoka sawa ila sijawahi hivi karibuni.
Wenye kujua tasfiri nisaidieni mwenzenu.