getrusa
JF-Expert Member
- Aug 16, 2013
- 2,150
- 1,824
Wakuu, naomba msaada kwa wajuzi wa kutafsiri ndoto. Nimekuwa naota tukio hili kila baada ya miezi fulani. Ndoto yenyewe ni kama hivi..:
Mwanzo niliota nimeenda kununua kiwanja cha kujenga mahali fulani kisha nikajenga nyumba sio kubwa sana na nikahamia na nilikuwa nahisi kabisa kuwa eneo lile nalifahamu na huwa naenda mara nyingi jambo sikumbuki ni wapi.
Ndoto ya pili: ni kama eneo lilelile nililo ota mara ya kwanza lakini safari hii nimejenga nyumba moja ambayo siyo nzuri sana lakini baadae nikanunua nyumba nyingine kisha nikanunue nyingine tena kisha nikajenga nyumba kubwa zaidi ya zile mbili.
Nikamfahamisha kaka yangu eneo hilo naye akaja akanunua viwanja eneo hilo hilo akajenga nyumba nzuri zaidi ya zile zangu na kubwa zaidi, hali hii ikawa kama halisi kabisa ninaweza kwenda na kurudi kwenye nyumba zangu na eneo nilifahamu kabisa. Ila sijui liko mkoa gani na wilaya ipi.
Na kila nikikataka kurudi katika ile nyumba ya kwanza kumbukumbu za mahali ilipo huwa zinapotea..
Ndoto hii ya kuota kuhusu nyumba imejirudia mara Nne kwa miezi tofauti nikiota eneo hilo hilo.. japo ki ukweli sijui liko mji gani na mkoa upi.
Ndoto ya tatu nimenunua shamba!
Kubwa kiasi lakini pembeni yangu kukawa na shamba jingine ambalo halijaendelezwa shamba pori kubwa zaidi nikalinunua,
Kaka yangu naye akaja akanunua kubwa zaidi yangu lakini kila nikitaka kurudi kwenye mipaka ya shamba langu la awali kumbukumbu zinapotea ama nakuwa siikumbuki mipaka. Ya shamba hilo
Na hii pia imejirudia zaidi ya mara tatu.
Kila nikijaribu kuwaza sipati majibu
Mwenye ujuzi wa ufasiri wa ndoto naomba msaada tafadhari..
Sent using Jamii Forums mobile app