Msaada tafadhali: Nimezaa nje, lini nimweleze mke wangu?

Msaada tafadhali: Nimezaa nje, lini nimweleze mke wangu?

Ivi nikuulize bro ingekuwa mkeo ndio kapata mimba ya yule jamaa yake ungejisikiaje??? nikweli mara nyingi hasira huwa haetendi haki siku zote, ndugu kaa na mkeo umweleze sababu ilio kufanya uchepuke kwanza na umueleze jinsi unavyo jutia kwa ulilofanya na umwombe msamaha, pili mjadili kuhusu matunzo ya mtoto kwangu mie naona ni vizuri kama mkeo akikusamehe mwambie na usimfiche mpaka hatua ulio nayo ili umchukue mtoto ukae nae umlee kama hatoka kubali basi mpeleke kwa wazazi wako ili wamlee mtoto. nakwambia ivi kwa kuwa kama mtoto akiendelea kubaki na mama uwezi jua huyo bint bado anamapenzi na wewe so mtoto itakuwa kigezo cha kuwa na wewe hilo litazidi kuhatarisha ndoa yako. jaribu kuongea na bi mkubwa ongea nae kama mkosaji sio kama mwanaume kichwa cha familia ubavu na amri. hata kama huyo msichana atafanya siri unazani mtoto atakuja kujua baba yake ni nani??. Bro sikunyingine kama unachepuka basi tumia kinga leo umempa mimba huyu kesho utapata majanga zaidi ya hayoo
 
Mkae mkijua kwamba mwanamke hata akiolewa huwa bado anajua kuwa kwao ni kwa baba na mama yake. Ndio maana hata ukimkorofisha itasikia akitishia kurudi kwao. Kwa akili ya haraka mwanamke ulienae hapo sio kwao. Mwanao uliemzaa kwa yoyote... awe beki3 malaya au mweu ni mzawa hapo kwako. Husikubali mtu wa kuja (mke) kumfukuza mzawa. Tafadhali leta mwanao bila kuogopa chochote maana hapo ndio kwao. Huyo wa kuja ana option nyingine (akae au arudi kwao) mtoto anayo option moja tu kakaa kwake.
 
Wengi wamekupa ushauri unaofanana fuata Kati ya hizo, akili za kuambiwa changanya na zako alafu unapata jibu kamili kisha unachukua hatua iliyo sahihi.
 
ikiwa wewe ni Mume wangu wala usije nieleza huo upuuzi. U better stay silence forever.
 
wanaume wanaumiza bas tuu....ulimsamehe then ukarevenge bado ukawa unamhudumia how far do we sure mmeachana?mm mtoto nikimkuta sna shda ila wa kunikuta anaumiza sana bas tuuu!ushaur wangu sisi wanawake wengne wana roho mbaya atanyanyaswa huyoo hasa km we upo busy mi nashaur asa hv mpeleke kwa wazazi wenu km wapo hai au ndugu zako akikua kianzia14 at least anajimudu ndo imchukue ukae nae ila kwa sasa mi sikushauri japo simjui mkeo.
 
sio ishu bana mlete mtoto home mwambie mkeo huyu ni mtoto

wangu full stop mpe vifungu vya bible watoto ni malaika

hawa kosa kujieleza kosa kwa mkeo kwani yeye ni Mungu

mchane live huyu ni mtoto wangu full stop

wala usimruhusu akuhoji ulimzaa lini ,kwsb hata ukwimbia ulimzaa lini it wont change anything

by the way mistake is human right
 
ikiwa wewe ni Mume wangu wala usije nieleza huo upuuzi. U better stay silence forever.

Hata kama ningekuwa mimi aise bora apige kimya na mapenzi yangeishia pale pale aende kwa beki tatu
 
HESHIMA beki3 (hgirl. Nikawa ananiletea mtoto nyumbani yeye ataenda kwao!

SASA SWALI: nifanyeje? niendelee na siri hii mpaka lini? Huyu beki3 anasema kama nikiwapa matunzo vizuri hana shida, ? Say 10+ years? How do you go about this?
Nawasilisha...
very simple mwambie pindi anachepuka na ww ulichepuka kidgo bahati nzuri wewe ukabahatika kupata copy, was not planned
 
Ukweli wako utakuweka huru,muombe msamaha mkeo,chukua mwanao maisha yasonge mbele.
 
Ulipomtafuta huyo kimada nje uliwaza lin utamwambia mkeo?
Kama HAPANA bas kausha ukimwambia kitakuwa kimbelembele chako.
Ila andaa kabisa WOSIA kabla huja R.I.P maana ushachanganya familia na kila mtoto ataangaza macho ktk hilo Vogy & Bangaloo
 
mbona ngoma rahisi tu, wewe mwambie wife kuwa wakati ule yeye aki cheat uligundua mapema na ukawa umechanganyikiwa na ukashindwa mwambia, ili kupoza moyo ndo ukagonga HG, tena mwambie uligonga mara moja tu, kisha baada ya kupata mimba hakukwambia kuwa ni yako, baada ya kuhamia mtaani na maisha yake kuwa magumu ndo amekwambia ukweli, sasa wewe zuga kwa wife kuwa huna uhakika kuwa mtoto ni wako kwa hiyo unataka kwenda kufanya DNA test ili kujua, mwambie kuwa lengo ni kuwa kama ni mtoto wako ili asiteseke na maisha ya shida, kama mkeo kweli ni muelewa lazima ataingia kingi na atakuona mtu mwenye huruma na mwenye kujali, akikasirika na kuja juu mwambie wewe ulivyogundua madudu yake ulikuwa mpole na ukakubali yaishe ili maisha yaendelee.

Duh
Aiseeeee nimekukubali
 
mpe mkeo ukweli japo utakuwa mchungu lakn mwarobaini ataumeza tu. japo atamaind mwanzon lakn atakuelewa baadae na mbembeleze kweli mpaka akuelewe kutoka moyoni ili hata huyo mtoto atapokuja kukaa hapo asije akamnyanyasa..
 
HESHIMA KWENU. MIMI NITA HILI JAMBO LINANITATIZA NA NAOMBA USHAURI WENU (PLEASE ONLY SERIOUS ADVICE) ESPECIALLY KWA WALIOKWISHAPITIA MKASA KAMA WANGU. NI HIVI:

Nimeoa nina watoto 3 na miaka 5 iliyopita niligundua mke wangu anaanza michepuka, nilikasirika sana na wakati nachunguza kujua ukweli, hapo nyumbani alikuwepo beki3 (hgirl) na siku nilipodhibitisha kuwa kweli mke wangu alikua na mpenzi (kabla yeye hajajua) nikaona kama nifanye revenge, nikamtongoza bk3 kiutani nikashangaa akawa mwepesi basi yaliyofata ndio hivyo. Nikawa kama nimenogewa. In the meantime nikampa live mke wangu kuwa ninajua anamchepuko fulani, akalia sana akaogopa sana akanipigia magoti akaomba msamaha na kusema hakuwa amefika mbali na jamaa na hivyo akaahidi ku cut-off. Na kweli ali cut-off.
Huku nyuma baada ya miezi miwili beki3 akaniambia ana mimba, lah haula.! Lakini anaogopa kurudi nyumbani kwake, mimi kwa imani niliyonayo siwezi kutoa mimba, dada zake wa mbali hapa Dar wakajua wakataka kuja juu hadi mke angejua (aibu ata kwa familia). Mwisho nikaamua kumpangia chumba uswahilini, na kumpa matunzo hadi alipojifungua. Kipindi fulani hali yangu kifedha ikawa mbaya matunzo shakani, akatokea jamaa mmoja akampenda, akamchukua akawa anaishi naye (wakati huo mtoto ana miaka 4). Juzi January huyu beki3 akajifungua mtoto wa huyo jamaa. Jamaa hili yake ya chini sana kiuchumi, mimi ndio na-foot almost 70% ya budget yao!! Sasa miaka ya karibuni jamaa anamyanyasa sana huyu beki3 pamoja na mtoto wangu hawajali kabisa. Beki3 sasa anataka atoke kwa huyu jamaa ananishinikiza nimpangie chumba akae alee watoto wake. Sasa mimi nitaleaje na mtoto si wangu? Halafu naogopa nikifanya hivyo atakua kama nyumba ndogo yangu!! Lkni ananisumbua sana anataka atoke kwa huyu jamaa anasema la sivyo basi ananiletea mtoto nyumbani yeye ataenda kwao!

SASA SWALI: nifanyeje? niendelee na siri hii mpaka lini? Huyu beki3 anasema kama nikiwapa matunzo vizuri hana shida, hata nisipompa ukweli mke wangu forever. Lakini najua at some point in the future mtoto huyu (wa kike) sitaweza kujificha hisijulikane kuwa ni mwanangu! Je kumwambia mke wangu sasa hivi ni bora zaidi au nisubiri hadi mtoto atakapokua mkubwa zaidi? Say 10+ years? How do you go about this?

Nawasilisha...

usikurupuke kulipiza kisasi wakat hujiamin.
Sasa kama zilikuwa hasira sasa unaogopa nn? Si uliamua unyama unyama?
Ulivyokuwa unatoomba kavu hukujipanga kwa matokeo?
Kutoomba utooombe ww halafu sisi ndio tukujibie hvi inakuja akilini kweli?!
Poor u
 
Maji yamekwishamwagika. Bora umweleze mkeo mapema na umchukue mtoto ili akulie katika familia aweze ku cope vinginevyo unatengeneza janga.
 
Aiseeeee
Nampenda Yesu ila inapofika hili suala huwa nakosa uvumilivu, naomba Mungu anisaidie coz mi km mi cwez pokea.mtt wa mtu.
Uwiiiiiiii
 
HESHIMA KWENU. MIMI NITA HILI JAMBO LINANITATIZA NA NAOMBA USHAURI WENU (PLEASE ONLY SERIOUS ADVICE) ESPECIALLY KWA WALIOKWISHAPITIA MKASA KAMA WANGU. NI HIVI:

Nimeoa nina watoto 3 na miaka 5 iliyopita niligundua mke wangu anaanza michepuka, nilikasirika sana na wakati nachunguza kujua ukweli, hapo nyumbani alikuwepo beki3 (hgirl) na siku nilipodhibitisha kuwa kweli mke wangu alikua na mpenzi (kabla yeye hajajua) nikaona kama nifanye revenge, nikamtongoza bk3 kiutani nikashangaa akawa mwepesi basi yaliyofata ndio hivyo. Nikawa kama nimenogewa. In the meantime nikampa live mke wangu kuwa ninajua anamchepuko fulani, akalia sana akaogopa sana akanipigia magoti akaomba msamaha na kusema hakuwa amefika mbali na jamaa na hivyo akaahidi ku cut-off. Na kweli ali cut-off.
Huku nyuma baada ya miezi miwili beki3 akaniambia ana mimba, lah haula.! Lakini anaogopa kurudi nyumbani kwake, mimi kwa imani niliyonayo siwezi kutoa mimba, dada zake wa mbali hapa Dar wakajua wakataka kuja juu hadi mke angejua (aibu ata kwa familia). Mwisho nikaamua kumpangia chumba uswahilini, na kumpa matunzo hadi alipojifungua. Kipindi fulani hali yangu kifedha ikawa mbaya matunzo shakani, akatokea jamaa mmoja akampenda, akamchukua akawa anaishi naye (wakati huo mtoto ana miaka 4). Juzi January huyu beki3 akajifungua mtoto wa huyo jamaa. Jamaa hili yake ya chini sana kiuchumi, mimi ndio na-foot almost 70% ya budget yao!! Sasa miaka ya karibuni jamaa anamyanyasa sana huyu beki3 pamoja na mtoto wangu hawajali kabisa. Beki3 sasa anataka atoke kwa huyu jamaa ananishinikiza nimpangie chumba akae alee watoto wake. Sasa mimi nitaleaje na mtoto si wangu? Halafu naogopa nikifanya hivyo atakua kama nyumba ndogo yangu!! Lkni ananisumbua sana anataka atoke kwa huyu jamaa anasema la sivyo basi ananiletea mtoto nyumbani yeye ataenda kwao!

SASA SWALI: nifanyeje? niendelee na siri hii mpaka lini? Huyu beki3 anasema kama nikiwapa matunzo vizuri hana shida, hata nisipompa ukweli mke wangu forever. Lakini najua at some point in the future mtoto huyu (wa kike) sitaweza kujificha hisijulikane kuwa ni mwanangu! Je kumwambia mke wangu sasa hivi ni bora zaidi au nisubiri hadi mtoto atakapokua mkubwa zaidi? Say 10+ years? How do you go about this?

Nawasilisha...

Haka kastory kakutunga katamu aisee....Mweleze tu wakati anatoka na jamaa na wewe uliamua kulipuka na beki3. Omba Mungu akusamehe then mkeo.
 
Aiseeeee
Nampenda Yesu ila inapofika hili suala huwa nakosa uvumilivu, naomba Mungu anisaidie coz mi km mi cwez pokea.mtt wa mtu.
Uwiiiiiiii

hahahaaa! Nmecheka sana.
Hlo ni kweli hata yesu aliisisitiza sana amri ya upendo. Utakuwa unamkosea mungu wako kwa kukichukia kiumbe kisicho na hatia.
Je kama ww ndio una mtoto na mmeo hana mtoto itakuwaje?
 
Back
Top Bottom