Habari ya jumapili Ndugu zangu, niende kwenye mada moja kwa moja. Mwaka Jana mwezi wa kumi na moja nilicheza US green card lottery na mwezi huu wa tano nimefanikiwa kupita katika mchujo wa kwanza unaofanywa na Kentucky Consular Center (KCC) niliingiza confirmation number katika website ya dvlottery.state.gov nikakuta barua kuwa nimefanikiwa kuchaguliwa, lakini ile barua inasema kwamba kuchaguliwa katika mchujo huu haimaanishi kuwa tayari nimepata visa hapana bado kuna hatua nyingine za kufuata ili kuwezesha kupata visa. Pia ile barua inasema kuwa kuna form inaitwa DS-260 Immigrant visa and Alien Registration Application, kwahiyo mpaka sasahivi bado sijaelewa hiyo form ninaipata wapi na baada ya hapo nini kitafuata?, je, ni vitu gani vya kuzingatia ili niweze kushinda na kupata visa. Msaada wenu ndugu zangu ni wa muhimu sana.
Cc: BAK, Nyani ngabu, Mzizi mkavu, ogah, masanja na wengine ambao wanafahamu mambo haya naombeni mniambie. Mbarikiwe sana.
Cc: BAK, Nyani ngabu, Mzizi mkavu, ogah, masanja na wengine ambao wanafahamu mambo haya naombeni mniambie. Mbarikiwe sana.