Msaada tafadhali kuhusu Mirathi

Msaada tafadhali kuhusu Mirathi

neyi

Member
Joined
Oct 13, 2014
Posts
8
Reaction score
0
Baba yangu alikuwa ni mwalimu,alifariki 2004 na mirathi ilitoka mwaka 2005 kipindi hicho tulikuwa wadogo hatukuwa tunafahamu sana kuhusu mirathi lakini aunt yetu ndio aliyekuwa msimamizi, mama hakushirikishwa kwa kiasi kikubwa kutokana na ndugu zetu kuwa wababe sana,mirathi ilitoka na kugawanywa walivyopenda wao mama hakusema kitu wala kupinga alikaa kimya na kusema ni mambo ya kidunia yanapita tu acha wafanye wapendavyo.

Tumekuwa kwa shida sana na mama yetu amekuwa mstari wa mbele kuhakikisha tunapata elimu kwani aliamini ndio mkombozi wetu.Kipindi chote wakati tunaomba mikopo bodi ya mikopo elimu ya juu tulikuwa tunaomba death certificate ya baba na kuambulia kupewa copy tu na aunt ambaye ndie msimamizi wa mirathi ukimuuliza original anakuwa mkali hatoi majibu mazuri.

Sasa mwaka huu mdogo wangu alikuwa anatuma maombi na mimi ndio nilikuwa namsaidia hivyo tukahitaji death certificate ya baba,nikampigia simu aunt akasema hana kama nina shida nacho niende mahakamani wakanipe nikamsihi sana akasema yeye alipewa pia copy original ilibaki mahakama ya mwanzo hawakumpa kumuuliza sababu za wao kukaa nacho ni nini hasemi ni mkali sana.

Basi nikamwambia anitafutie hata copy tu akadai nimpe pesa akakifuatilie nikampa akaja na copy sikusema kitu ingawa kwenye kucertify vyeti walitaka original nilipata shida sana kuwaelewesha.

Siku moja mama kanipigia simu akaniambia aunt amemfuata na kumwambia kuna pesa ambayo mama mjane anatakiwa kupewa kila mwezi kwa ajili ya kujikimu na alitakiwa apewe toka baba alipofariki hivyo afanye madai ya miaka yote,pesa hiyo imeleta ugomvi mkubwa sana kwakuwa aunt anadai igawanywe na pesa yenyewe si nyingi kivile,nimemshuhudia mama yangu akipata shida miaka yote leo hicho kipesa kidogo ambacho ni haki yake kigawanywe tena hiyo ni haki kweli??.

Kwa wenye uelewa je,nyuma ya hiyo death certificate ya baba yangu kuna nini kinaweza kuwa chanzo cha cheti hicho kubaki mahakamani?.

Na je,mbali na mirathi na hiyo pesa ya mjane je,inawezekana kuna madai mengine yapo ambayo hatuyajui?
nilisikia watoto chini ya miaka 18 huwa wanapewa pia mafao je, ni kweli??.

Nawasilisha kwenu wadau.
 
Pole sana kwa mambo magumu unayoyapitia na mwenyezi mungu atawasaidia.
Ngoja waje wakupe msaada.
 
Huyo aunt yenu aalaaniwe na Mungu. Mtoto hata akiwa na mwezi mmoja mafao ni haki yake kisheria.
 
Pole sana mdogowangu neyi kwa masahibu hayo,muombeni mungu atawavusha katika kipindi hiki kigumu.Wewe unaishi mkoa gani,kama upo hapa Dar fika ofisi za Tamwa,Sinza Mori au ni PM nione nitakusaidiaje.
 
Unaweza kwenda mahakamani kupata copy ya mirathi au mkacertify hiyo mli yo nayo. Ila itabidi mumshirikishe aunt yenu kwenye baadhi ya maeneo sababu yeye ndio msimamizi wa mirathi.

Mnaweza pia kukaa kama ndugu na kupeleka Malalamiko yenu kwa ukoo na baadaye mahakamani kuhusu aunt yenu na kuomba abadilishwe.

Msimamo hana mamlaka ya kumiliki bali ni administrator tu wa mali.

Ni haki yenu kupewa original na mahakama.
 
Haki za marehemu kwa mwaka 2004 zinapatikana ktk mfuko wa PSPF ambapo wanatoa kiinua mgongo km death gratuity na monthly pensions kwa wategemezi. Pamoja na mwajiri kumlipa hela ya kusafirisha mizigo ya marehemu kutoka alikofia kwenda kwake.
Ushauri wasiliana kwanza na PSPF sehemu yeyote watawapa taarifa sahihi na ushauri pia mshirikishe mwajiri wake wa mwusho.
Otherwise poleni sn
HRO by professional
 
asanteni kwa ushauri wenu nitaufanyia kazi,mbarikiwe jamani nitaleta mrejesho mambo yatakavyokuwa.
 
Back
Top Bottom