mpenda arage
JF-Expert Member
- Nov 10, 2015
- 1,677
- 3,806
Habari zenu wakuu. Samahani hivi kuna mdogo wangu amenieleza kuwa, kuna chuo kinapatikana Dar es Salaam. Ambacho kinatoa kozi fupi za uhudumu wa maofisini, ambapo wanakutafutia sehemu za kufanya field, na ukishamaliza wanakutafutia sehemu ya kufanyia kazi wao wenyewe. Na ameongezea kuwa utakapopata kazi katika hizo ofisi, unao uwezo wa kupata kazi humo humo kama una ujuzi mwingine na ukaajiriwa kabisa. Kifupi yeye ana degree ya HR kwahiyo kuna mwenzie amemshawishi kusoma hizo kozi fupi. Ili wakishapata hivyo vibarua, baadae aje afanye mchakato wa kubadilikia humo humo! Kwakuwa mimi hizo taarifa ni ngeni masikioni mwangu. Ndio maana nimekuja hapa kwa wajuvi wa mambo. Isije anaenda kujipausha tu huko! Na nitafurahi zaidi kama mtanitajia na majina ya hivyo vyuo. Nitanguliza shukran zangu kwenu.
Sent using Jamii Forums mobile app
Sent using Jamii Forums mobile app