Msaada tafadhali: Controller and Auditor General (CAG) ni nani kwa mujibu wa Katiba ya JMT?

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,968
141,979
Nafikiri tukijua dhamana aliyonayo CAG kikatiba pamoja na majukumu yanayomzunguka itatusaidia sana siku za usoni kufanya rejea.

Nauliza swali hili baada ya kukumbuka kuwa wakati fulani katika bunge la mama Makinda mbunge wa ubungo mh JJ Mmyika alidai bungeni kuwa Rais Kikwete ni dhaifu ( ipo tofauti kati ya Rais Kikwete na mh Kikwete). Sikumbuki Mmyika alichukuliwa hatua gani ila ninachofahamu ni kuwa mbunge ana kinga azungumzapo akiwa bungeni.
Kadhalika sikumbuki kama mstaafu Kikwete alitunisha msuli kuwa kadhalilishwa.

Kwa kuwa tupo hapa jamvini kujifunza pia, naomba nijibiwe swali langu tafadhali.

Maendeleo hayana vyama!
 
Ngoja wanasheria waje ila nimesikia spika Sasa hivi anahojiwa BBC aisee sikuwahi kujua ndugai hana busara Na mfinyu wa akili kiasi hicho!
 
Sasa CAG mwenyewe hata kufukuzika hafukuziki sijui mtu wa aina hii unamwita kumhoji ili nini ukizingatia alichosema wala sio jinai. Badala ya kufuatilia mambo ya msingi wanayapa uzito mambo ya kipumbavu halafu nchi iingie uchumi wa kati; sio kwa upumbavu huu.
 
Sasa CAG mwenyewe hata kufukuzika hafukuziki sijui mtu wa aina hii unamwita kumhoji ili nini ukizingatia alichosema wala sio jinai. Badala ya kufuatilia mambo ya msingi wanayapa uzito mambo ya kipumbavu halafu nchi iingie uchumi wa kati; sio kwa upumbavu huu.
Spika angeweza kumuita chemba mzee mwenzie wakayamaliza kiutu uzima bila tension kama hii ya sasa.

Hapa naona bifu kama la bosi wa Takukuru na DPP enzi za JK kurushiana lawama huyu hafanyi kazi yake kwa kesi tunazo mpelekea ndio maana mafisadi hawachukuliwi hatua kwa wakati.
 
Back
Top Bottom