kuna tablet za windows hizi ni nzuri kama utakuwa unatengeneza documents, zenyewe unaweza tumia modem, keyboard, mouse nk ukiwa umetulia na unatumia kama tablet ukiwa kwenye mizunguko. maarufu zake ni
-dell venue 8 pro
-lenovo miix au yoga
-asus vivotab note
-toshiba encore
hizo tablet zinakuwa na specification tofauti hivyo hakikisha ukienda kununua inakuwa na ram 2gb na storage kuanzia gb 32. zipo variety za 1gb zinauzwa bei rahisi sana euro 99-120 lakini 1gb itakukwaza sana.
pia ukinunua tablet ya windows ununue na usb hub sababu inakuwa na port 1 tu, hii usb hub unaichopmeka kwenye hio port 1 then unapata port nyingi kwa ajili ya kuchomeka vitu vyengine
incase umeshindwana na windows tablet, zipo za android pia angalia
-samsung galaxy tab 4 7inch zinapatikana budget hio
-kama ni lenovo hakikisha inaanziwa na yoga au thinkpad
-asus pia ana tab za bei rahisi za android
ukitafuta vizuri unaweza pata ipad mini ya kwanza kwa bei hio pia.
kama unatumia website za online au duka unalonunulia lina website unaweza nitumia link nikaangalia bidhaa zao then nikakuambia ipi nzuri