Msaada simu yangu bar za network zimepotea

Msaada simu yangu bar za network zimepotea

ivunya

JF-Expert Member
Joined
Sep 18, 2015
Posts
2,290
Reaction score
2,230
Hii Leo ni Siku ya pili bar za network zimepotea ghafla , nashindwa kuelewa tatizo ni nini kila laini ninayo weka bar za network zinatokea kuashiria kuwa lain ipo kwenye simu ghafla zinatoweka ndo basi tena hazirudi naandikiwa NO SERVICE-HALOTEL. Nikawa nawaza Wenda imefungia lakin nikitumia Huduma ya WIFI katika simu hiyo hiyo inaendelea kufanya kazi kuingia katika INTERNET. Hata hii post nimeandika katika simu hiyo hiyo kutumia WiFi. nikiweka lain yeyote ile ina detect lakin bar za network zinatoweka. Nilikuwa naomba msaada tatizo ni kitu gani? naipenda simu yangu
 
Piga *#06# alaf lete majibu ,
Nb: weka namba nane tu za mwanzo kwa usalama
http://
Pia toa taarifa za simu kama brand, na model yake
 
Angalia unaweza kuwa umebonyeza kitufe kama hiki [emoji574][emoji574]bahati mbaya huwa kinakata network [emoji574]
 
Angalia unaweza kuwa umebonyeza kitufe kama hiki [emoji574][emoji574]bahati mbaya huwa kinakata network [emoji574]
Ndugu hicho kitufe sijabonyeza . yaan ukiweka lain zile setting zinatokea change za kuset data connection ghafla bar zinatoweka.
 
Jaribu kubadilisha NETWORK MODE--->>>> GSM ~~~~~>>>>from --->>WCDMA.
 
Jaribu kubadilisha NETWORK MODE--->>>> GSM ~~~~~>>>>from --->>WCDMA.

Sony Xperia yangu ikiwa WCDMA network bars hupotea, lakini ikiwa GSM ipo mwaya mwaya,japo situmii 3G.
 
Mkuu na tatizo la simu kushindwa kuonesha video ,picha pia PDF huwa linasabishwa na nini?


PDF lazima u_download application inayosoma PDF file, kwa mfano mimi natumia Office Suite.

Kuhusu kutoonyesha video,sina uhakika. Wewe hutumia application gani kufungua videos??? Mimi nina VLC,MX PLAYER na KM PLAYER. Jaribu hizo au mojawapo halafu ulete feedback.
 
Piga *#06# alaf lete majibu ,
Nb: weka namba nane tu za mwanzo kwa usalama
http://
Pia toa taarifa za simu kama brand, na model yake

Mkuu, hivi ukipiga hiyo number kama namba haijatoka inakuwa ndio imefungiwa na tcra au ikifungiwa hata imei number inakuja kama kawaida...?.
 
Kk ucangaike TCRA wamefanya yao niamimi nina ushaid
 
Back
Top Bottom