Msaada: Simcard huwa inakula data?

josephwaara

JF-Expert Member
Jun 18, 2016
304
637
Wakuu heshima kwenu.

Kuna jamaa angu analalamika ulaji wa wa data kwenye simu yake, unaweza kukuta 2gb sinakata mchana mmoja tu ila matumizi yake anadai ni ya kawaida tu.

Nilipocheki Data Usage kwenye simu yake niliona kinachotumia data kwa wingi ni "Simcard Traffic ." (Sikumbuki vizuri maneno yote).

Msaada wenu katika hili wakuu, hiyo traffic ndo nini na tufanyeje kuirudisha simu normal?
 
SIM card haili traffic SIM card ni njia ya kukutambilisha wewe kwa mobile operator wako kwa njia salama ajue kuwa kweni ni wewe na akupe access ya network na account yako.

Ni vizuri ungesoma vizuri maneno yaliyoandikwa na ufanye uchunguzi zaidi, kwa mfano ukienda kwenye Mobile data usage kwenye simu ya samsung itakwambia app zinatumia data kiasi gani kisha ukigusa hizo app itakupeleka kwenye detail zaidi ya hizo app. Pia anaweza kujaribu app kama GlassWire Data Usage Monitor ambayo itaonuyesha data zinaenda wapi.

Kuna matatu tu hapo;
  1. Haelewi matumizi yake ya data vizuri, mtu anaangalia Insta/TikTok siku nzima halafu anasema hana matumizi makubwa, anarekodi video ambazo zinafanyiwa backup Google Drive etc.
  2. Kuna App/apk ameinstall kutoka sehemu zisizoelewa GBWhatsApp etc ambayo inafanya mambo yake yenyewe.
  3. Bug kwenye app halali ambayo inadownload data kupitiliza.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom