usisome php... we nenda na
HTML/CSS -> Javascript (Core na NodeJS) -> MYSQL/MONGODB
usome Nodejs badala ya php kwa sababu:
Kwanza ni javascript kwa hiyo hupotezi muda kusoma language mpya "php",
Pili ni rahisi sana kutengeneza site from zero hadi ikakamilika kwa muda mfupi sana kuliko php, site inayoweza kukuchukua mwezi kwenye php itakuchukua robo ya muda kwenye NodeJS,
Iko faster kwenye kazi nyingi sana kuliko php, ni full non-blocking io unlike php ni blocking io inachukua kazi sana kuandika nonblocking io script kwenye php...
Kingine kwa kua NodeJS ni javascript kuhandle JSON ni rahisi sana sababu ni kama native kwenye javascript, unlike kuparse json kwenye php inakua mziki zaidi...
Bado nodeJS inaweza kuhandle concurrent users wengi sana kuliko php, mfano kuhandle watu elfu kumi kwa wakati mmoja unaweza chomoka kirahisi sana kwenye machine moja unlike php utahitaji kuongeza server.
Faida ni nyingi kwa leo niishie hapo....