Unaweza tumia option kadhaa
1. Install wine. Hii program inapatikana ndani ya ubuntu software center itakuwezesha kurun windows programs direct kwenye ubuntu. Kasoro yake ni kwamba some programs zinaweza kuwa incompatible na huwa hazi look good kama native program za ubuntu or zinavyokuwa kwenye Windows. pia unaweza install playonlinux kwa ajili ya kuplay games za windows
2.Tumia virtualbox. Kama PC yako ina spec nzuri (4GB+ RAM na processor modern kama i3/i5/i7) unaweza install windows OS ndani ya ubuntu na ikawa kama program. Ndani ya hiyo windows ndio utainstall programs za windows bila shida yoyote. Faida yake ni kuwa programs za windows almost zote except games zinarun bila shida na zinalook good, pia unakuwa na uwezo wa kutumia OS zote mbili bila kuzima PC yako. Disadvantages zake ni kuwa haiwi faster kama inavyorun direct kwenye hardware. Na vitu kama games (3D) inakuwa shida kuziplay
3. Dual booting. Hii ni kuistall OS mbili kwenye pc na unakuwa unachagua ipi utumie unapowasha PC yako. Hii haina shida yoyote kwa upande wa programs, ila ukitaka kutumia OS moja nyingine inakuwa Off