Msaada pls | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msaada pls

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Joyceline, May 18, 2011.

 1. J

  Joyceline JF-Expert Member

  #1
  May 18, 2011
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 1,010
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  mdogo wangu anafunga ndoa mwezi wa tisa, tupo kwenye process ila jan amegundua mchumba wake ana mwanamke na mtoto mchanga wa miezi mmitatu wamefanana kama mapacha, alizaa naye akiwa arusha amemleta dar amempangia nyumba ila jamaa ni smart imetumika trick kali sana kumnasa, mdogo wangu amechanganyikiwa sana nimemwambia kila neno nmechoka, embu nipeni tips za kumsaidia, ndani hakupikwi wala hakuliki.
   
 2. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #2
  May 18, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Aiseeee...sasa kuna ndoa hapo kweli???!Nwy wakae waongee maana kuna
  nnaemjua ana mtoto wa miezi kadhaa na mwezi wa saba anafunga ndoa na mwanamke mwingine..mke mtarajiwa kakubali kwakua kaambiwa mwenzie hapendwi ilikua tamaa tu!!
   
 3. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #3
  May 18, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Huyu jamaa sidhani kama ana nia nzuri na mdogo wako yaani hadi kampangishia nyumba huyo mwingine nafikiri cha msingi ni kuweka kikao na kujua black and white kuhusiana na hili suala otherwise anakoelekea atalia vilio vingi zaidi ya ambavyo analia sasa hivi
   
 4. M

  Marytina JF-Expert Member

  #4
  May 18, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,034
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  why BOYS are like this?
   
 5. J

  Joyceline JF-Expert Member

  #5
  May 18, 2011
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 1,010
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Mimi nimemshauri aachane naye, maana jamaa tangu jana hajasema chochote na kwenye simu hapatikani, sasa mdogo wanguananiuliza nimsrudishie vitu vyake eg. engagement ring nk maana ni ujinga kuvaa engegement mtu ana mwanamke tayari , halafu wala hajuti, huyo dada alikuwa anakaa arusha akamuhamishia dar, ili awe karibu na mtoto wake kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari. ndo mtoto wake wa kwanza, mdogo wangu alikuwa na matatizo ya tumbo la uzazi ila alishatibiwa kwa hiyo aliwahi kubeba mimba mbili zikatoka, nadhani jamaa akaamua kujaribu kwingine
   
 6. J

  Joyceline JF-Expert Member

  #6
  May 18, 2011
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 1,010
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Wako pamoja tangu 2002 mpaka leo, hajawahi kuwa na mwanume mwingine zaidi ya huyo, kwa ufupi hamjui mwanaume mwingine zaidi ya huyo mchumba wake. tangu mdogo ameumia sana
   
 7. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #7
  May 18, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Are like what???
   
 8. J

  Joyceline JF-Expert Member

  #8
  May 18, 2011
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 1,010
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  amelia kuanzia jana saa 10 jioni mpaka saa 11 asubuhi, nalala, naamka namkuta analia nimetoka kwenda kazini hajalala, na mchana huu napiga simu analia tu BP imeshuka
   
 9. Mkimbizi

  Mkimbizi JF-Expert Member

  #9
  May 18, 2011
  Joined: Aug 23, 2008
  Messages: 222
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  is because we are boys
   
 10. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #10
  May 18, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  8 years jamaa anakuja kumpotezea mdogo wako muda, mwambie atulie tu kwanza.
   
 11. J

  Joyceline JF-Expert Member

  #11
  May 18, 2011
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 1,010
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Mnajua kutuumiza sana
   
 12. Kbd

  Kbd JF-Expert Member

  #12
  May 18, 2011
  Joined: Oct 9, 2009
  Messages: 1,264
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  Sijui kwa nini idadi ya kina shoziniga inaongezeka kwa kasi hivi:mod:
   
 13. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #13
  May 18, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Aiseee bora amuache...inaonekana jamaa anatafuta mzaaji tu na sio mapenzi haswa!!Atafute bahati yake pengine maana hapo ikitokea akakubali kuolewa nae alafu asipate bahati ya kuzaa atanyanyasika sana bila kusahau masimango!!!
   
 14. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #14
  May 18, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Mwambie aache kulia banaa wanaume wapo wengi sana ya nini kumlilia mwanaume who's not worth it.
   
 15. Mkimbizi

  Mkimbizi JF-Expert Member

  #15
  May 18, 2011
  Joined: Aug 23, 2008
  Messages: 222
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  dah! ushauri hapo huyo mdogo wako aachane na huyo jamaa. Arudi kwenye dini haswa! Mungu atampatia mume mwema tu
   
 16. M

  Marytina JF-Expert Member

  #16
  May 18, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,034
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  like huyu mme mtarajiwa with a wife+child kisirisiri.
   
 17. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #17
  May 18, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Hapo mimi simo ng'o
   
 18. J

  Joyceline JF-Expert Member

  #18
  May 18, 2011
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 1,010
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Kaka yangu hakuna neno sijaongea, maneno yameniishia , nikirudi nyumbani sijui nitasema nini, namuonea huruma. analia
   
 19. M

  Marytina JF-Expert Member

  #19
  May 18, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,034
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  ombea hujazaliwa wa kike
   
 20. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #20
  May 18, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Huyo ni a BOY not a MEN.
   
Loading...