Unatakiwa uwe na simu yenye bluetooth na uweze kuzi pair na hiyo headset ili iweze kufanya kazi. Kama unayo simu ya bluetooth, nenda kwenye option ya bluetooth, unaiwasha bluetooth ya simu, na bluetooth headset yako uiwashe iwe kwenye pairing mode. Kwenye simu unakwenda kwenye option ya 'search for devices'. Simu ikishaiona hiyo headset, unatakiwa uweke password ya hiyo headset. Mara nyingi ni 0000. Ikishaisoma utaona ujumbe 'paired', na hapo unaweza kuitumia hiyo headset.
Natumaini nimeeleweka.