Msaada: PC yangu haiwaki

Msaada: PC yangu haiwaki

Bruce Hebrews

Member
Joined
Sep 22, 2021
Posts
17
Reaction score
35
Habari zenu ndugu zangu Nina PC Aina ya HP niliiweka kwenye Chaji Usiku Sasa asubuhi nimeamka naona Haiwaki kabisa, vilevile Button ya Kuwashia PC naona imekuwa inatoa ka MWANGA hafifu nimejaribu kuiweka kwenye soketi nione Kama Itawaka au Laa lakini mpaka Sasa bado. Anayejua Tatizo litakuwa Nini Msaada jaman

View attachment 2029080
 
Toa Batery,Disconnect cables zote kisha bonyeza kitufe cha kuwashia kwa sekunde 30 uachie then weka batery washa maisha yatakuwa laini.
 
Matumizi mazuri ya PC ni
  • Ukimaliza kutumia, zima au sleep
  • Disconnect waya zote km adapter n.k
  • Chomoa vifaa vyote modem n.k
  • Battery ikijaa, chomoa adapter
Hiyo siyo simu kwamba uweke chaji usiku mzima.
Toa battery, rudishia kisha angalia km kuna taa nyekundu pembeni mwa pc inaonyenya moto inapitisha. Subiri km dk 10
Washa computer yako kisha bonyeza windows button + f5
 
Matumizi mazuri ya PC ni
  • Ukimaliza kutumia, zima au sleep
  • Disconnect waya zote km adapter n.k
  • Chomoa vifaa vyote modem n.k
  • Battery ikijaa, chomoa adapter
Hiyo siyo simu kwamba uweke chaji usiku mzima.
Toa battery, rudishia kisha angalia km kuna taa nyekundu pembeni mwa pc inaonyenya moto inapitisha. Subiri km dk 10
Washa computer yako kisha bonyeza windows button + f5
Asante Kaka
 
Hujasema kama screen inawaka au haiwaki au zile taa zinawaka vipi.

Kikawaida pc ikijaa basi inaacha kuchaji yenyewe hata kama hujachomoa waya, hiyo yako naona haina hiyo system hivyo imesababisha kuovercharge.
Hata hivyo hilo hapo juu linaweza lisiwe tatizo.

Sababu kuna factory nyingi zinazoweza kusababisha pc isiwake na kugundua tatizo mara moja inaweza kuwa kazi kama huna experience binafsi au utundu wa kuzaliwa. so solution ni kujaribu kila option.

Chomoa battery ya pc iweke pembeni kwa dk30 mpka saa1.
Wakati unasubiri huo muda upite bonyeza power button kwa dk1, then chukua adapter chomeka kwenye pc na ujaribu kuiwasha bila ya battery.

Ikiwaka basi jua tatizo ni battery na kama ikigoma basi jaribu option nyingine.
Sasa hivi chukua battery baada ya dk30 au saa1 kupita na uiweke kwenye pc na ujaribu kuiwasha.
Ikigoma.
Basi jaribu kuchomeka adapter na uangalie kama chaji inapeleka na ujaribu kuiwasha.

Ikigoma tena.
Basi chomoa battery na adapter then toa RAM isafishe, then jaribu kuchomeka waya wa pc alafu iwashe.
Then zima pc na uweke RAM na ujaribu kuwasha tena.

Ikigoma basi jaribu option nyingine.
ONYO: Hii option ya mwisho ni ngumu na kama hujiamini au unaona huna uzoefu wa kufungua pc nzima basi ACHA WALA USIJARIBU sababu unaweza kutengeneza matatizo mengine mengi zaidi. mfano unaweza kusababisha shoti kwenye motherboard kwa kuigusa tu bare hands.

Ila kama unajiamini basi fanya hivi.
Anza kwa kuchomoa RAM, BATTERY, ADAPTER NA KILA KITU na ufungue pc yote.
Then jaribu kutoa CMOS battery then kaa kwa saa 1 then irudishe tena, chomeka ram, battery na adapter then washa pc.
Hii battery inaweza kuwa ndani kabisa ya pc attached kwenye motherboard kutegemea na pc.
Hapa utakuwa umefanya BIOS restoration manually hivyo kuna uwezekano mkubwa wa pc kuwaka kama tatizo litakuwa huko.

Vinginevyo PC yako itakuwa umeikaanga wakati unaichaji usiku au ili overheat na kuburn baadhi ya components kama uliiweka sehemu yenye joto sana.
Au umeme ulipiga shoti na kuharibu pc.
Kamwe usiweke pc kwenye chaji wakati wa usiku au ukiwa umelala sababu utakuwa hujui kinachoendelea na umeme unaweza kufanya yake wakati wowote considering umeme ulivyokuwa hovyo hivi karibuni.

Solution ya mwisho au ya kwanza ni kupeleka kwa fundi.
Mimi ni ya mwisho sababu napenda kuharibu na kufix mwenyewe ili nikijue kitu kiundani zaidi na sipendi ile ya kufanyiwa tu na fundi bila kujua kinachoendelea hii inapelekea wengi kupigwa.
Ndio maana mimi sijawahi kupeleka pc kwa fundi hata siku moja huwa nafight mwenyewe na hata nikipeleka basi fundi hatonipiga labda nimpige yeye.
JF itakusaidia sana kabla ya kupekeleka kwa fundi ila Google ndio mwisho wa matatizo.

Mimi pc yangu iliwahi kuzima mwezi mzima nikajaribu kila kitu ikashindikana nikahisi labda motherboard imeungua na niliifungua sana nikachomoa kila kitu kwake.
Ila tatizo nilisababisha mwenyewe sababu nilijaribu kufix fan ilikuwa inazingua mwishowe ikazima.

Ila siku moja niliifungua nikachomoa motherboard nikakuta bonge la vumbi, nikaisafisha kwa kitambaa then nikafanya hiyo option ya mwisho nikakaa kama saa1 moja nikafunga kila kitu Nikaipiga kwa joto la upepo kwa kutumia hand dryer ili nishtue processor na gpu ile nachomeka adapter na kugusa power button ikawaka nilihisi kama miujiza sababu nilichanganyikiwa kwa stress.

Mpaka leo sijui tatizo lilikuwa ni nini exactly lakini inapiga kazi mwezi 5 huu bila tatizo lolote.
Ila bila shaka nilizingua kwenye power supply consumption lakini wanasema if it works don't touch it.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom